KIJANA
mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Abdul mwenye umri wa miaka 20, Mkazi wa
Ilboru jijini Arusha, anatuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa mashuhuda, Abdul, mkazi, mapema leo hii (dec 3), alimwita
chumbani mwake mtoto wa mpangaji mwenzake (jina tunalihifadi) na kisha
akamfanyia kitendo hicho cha kinyama.
Wapangaji
wenzake waliposhtukia tukio hilo la ubakaji, walivamia chumba chake na
kumshushia kipigo kikali kabla ya kumpeleka kituo kikuu cha
polisi,Jijini Arusha.
Mtoa
habari wetu alisema mtuhumiwa alipohojiwa na polisi alikiri kuwa ni
kweli alimbaka mtoto huyo kwa kisingizio eti alipitiwa na shetani.
Hata
hivyo majirani wa Abdul wanasema hiyo imekuwa ni kawaida yake
kujihusisha na vitendo vinavyohusiana na ubakaji na tayari ana kesi
nyingine makahamani kwa tuhuma hizo hizo za ubakaji.
Saluti5 ilifanikiwa kufanya
mahojiano na mama mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la
Mariam akiwa ndani ya wodi namba 9 katika hospitali ya mkoa (Mount
Meru) ambapo alikiri binti yake kufanyiwa ubakaji na mpangaji mwenzake.
Akiongea huku akitokwa na machozi pembeni ya kitanda alicholazwa mwanae, Mariam alisema bado hajajua hatma ya afya ya mwanae
0 comments:
Post a Comment