Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa
--
Baadhi ya Maazimio
1.KIKAO cha kamati kuu kilikuwa cha kawaida ,hakuna jambo la dharula.
2.Mchakato wa katiba mpya usiathiri mabadiliko ya sheria nyingine kama mabadiliko ya sheria ya uchaguzi
3.Mwaka 2013,ni mwaka wa nguvu ya
umma,hakuna kubembelazana na serikali.rais kikwete hajajibu madai ya
CHADEMA kwa hiyo atashinikizwa.
4.sehemu ambazo CCM wanaogopa kuitisha uchaguzi,wanalazimishwa kuitisha uchaguzi.kata za arusha mjini,sengerema,nk.ziko 15
5.Uongozi wa KARATU wa CHADEMA
umesimamishwa kwa muda mpaka chama kitakapokamilisha uchunguzi wake
huko.wanasheria Marando na Prof Safari watachunguza kashfa za mtu
mmojammoja huko karatu.,
..........xxx...........xxx..................xxx............
Aliyekua Mwenyekiti wa Tawi la Chadema UK, Chris Lukosi Aelezea Kisa Cha Yeye Kuondoka Chadema na Kurudi CCM...''
Bw. Chris Lukosi
--
Leo hii nimeamua rasmi kurudi CCM, chama ambacho nimekifahamu kwa miaka 35 sasa.
Nilijiunga na Chadema kwa matumaini niliyokuwa nayo kuwa ni chama
kitakachomkomboa Mtanzania kutoka kwenye umasikini na kumfikisha kwenye
level sawa na watu wa mataifa mengine kama Botswana , Namibia au hata
baadhi ya nchi za Ulaya.
Niliamua
haya baada ya kufuatilia yanayoandikwa kwenye vyombo vya habari kwa
sababu mie binafsi kwa sasa naishi UK hivyo basi mambo mengi yatokeayo
nyumbani huwa nayapata kwa kusoma magazeti na blogs mbali mbali.
Nilifanikiwa
kukutana na Mheshimiwa Lema hapa London ambapo tukapanga mikakati ya
kukijenga chama hapa UK na nikapewa jukumu la kufungua matawi nchi nzima
na kuhamasisha Watanzania, kazi ambayo niliifanya kwa moyo mmoja. Pia
nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chadema UK.
Nimefanikiwa kuhamasisha watu wengi na baada ya miezi michache niliamua
kwenda nyumbani kuona hali ilivyo. Niliyoyakuta ilikuwa tofauti na
niliyokuwa nikiyasikia na kusoma.
NIMEKUTA BARABARA NZURI SIJAWAHI KUONA TOKA NIZALIWE NA ZINAENDELA KUJENGWA!
SHULE ZA SEKONDARI KILA KATA NA VYUO VIKUU VYA KUJICHAGULIA.
MAISHA
YA WATANZANIA YAMEBADILIKA SANA - MIDDLE CLASS NI MAISHA YA KAWAIDA TU.
VIJANA WENGI WAMEENDELEA TOFAUTI NA ZAMANI MPAKA UWE MCHAWI KIDOGO NDIO
UWE TAJIRI. MIJI INAJENGEKA KWA KASI YA AJABU.
UKIHARIBU KAZINI UTAWAJIBIKA .
Na mengine mengi tu niliyaona mpaka nikaanza kujiuliza , hivi najiita mpinzani, NINAPINGA NINI?
Kama ni maendeleo nayaona tena maendelo original Nikakumbuka msemo mmoja...
“KWA NINI UHANGAIKE NA FOTOKOPI WAKATI ORIGINAL IPOO?”
Kwangu
mimi CCM ni original na Chadema ni photocopy, tena copy iliyotolewa
wakati mashine imekwisha wino . Mabadiliko ya kweli yatatokea ndani ya
CCM na si kwingineko!
Kuna
mengi mazito yamenichefua Chadema lakini sitayasema leo. Juzi
mwenyekiti wangu wa Taifa Mheshimiwa Mbowe alipita hapa UK, lakini,
mpaka ameondoka hakutaka kuwasiliana na kiongozi yoyote wa Chadema hapa
UK kitendo ambacho kiliniuma sana, kwani, niliona kama tumedharauliwa;
BABA HUWEZI KWENDA SEHEMU WALIPO WANAO UKASHINDWA HATA KUWAPIGIA SIMU KUWAJULIA HALI.
Ni
matumaini yangu kuwa uamuzi wangu utaeleweka. Kama tujuavyo, kila
kwenye msafara wa mamba na kenge wamo, lakini naona kwenye msafara wa
Chadema idadi ya kenge inazidi mamba.
0 comments:
Post a Comment