Na Joseph Ngilisho -Arusha
Mwanafunzi
wa darasa la tatu katika shule ya msingi Sombetini mwenye umri wa miaka 10
(jina limehifadhiwa) jijini Arusha,amelazwa katika hospital ya mkoa Mount Meru
baada ya kubakwa na kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri na mwanaume mwenye
umri wa miaka 40 ambaye ni mtoto wa diwani.
Akizungumza
na vyombo vya habari mama mdogo wa mtoto huyo ,Fatuma Zuberi alisema kuwa tukio
hilo ambalo
limethibitishwa na jeshi la polisi jijini hapa,limetokea novemba 30 mwaka huu
majira ya saa moja jioni nyumbani kwao mtaa wa Pangani jijini hapa.
Akisimulia
zaidi alisema kuwa siku ya tukio yeye na familia hapo nyumbani walienda kwenye
sherehe za kicheni pati na kumwacha mtoto huyo nyumbani akiwa na bibi yake.
Alisema
kuwa baada ya kutoka katika sherehe hiyo majira ya saa 4 usiku walimkuta mtoto
huyo akiwa amelala chumbani bila kuwa na nguo ya ndani na kumhoji ,hata
hivyo mtoto huyo alisema kuwa hakuvaa chupi kwa kuwa ilikuwa inambana.
Alieleza
kuwa alimwamuru mtoto asilale bila kuvaa nguo ya ndani na kumtaka achukue nguo
hiyo avae ,hata hivyo alipigwa na butwa baada ya kuona nguo hiyo ikiwa mbichi
imetapakaa mbegu za kiume na damu, ndipo aliposhtuka na kutaka kumwadhibu mtoto
huyo,kutokana na mtoto huyo kutotaka kueleza kilichotokea.
Aliongeza
kuwa aliamua kumchapa ndippo aliposema ukweli kwamba alibakwa na mwanaume
aliyemtaja kwa jina la Thabit Jafari(40) ambaye ni jirani yao na ni mtoto wa
diwani wa kata ya mjini kati(ccm),Abdulrasul Tojo.
‘’tulishangaa
baada ya kuelezwa kuwa Jafari ndiye aliyehusika kumbaka mtoto wetu hatukuamini
kwani kijana huyo ni jirani yetu na tumekuwa tukiishi naye kwa muda mrefu kama ndugu na kwamba huyo anafamilia yake na anamtoto wa
kike anayesoma kidato cha tatu’’alisema Fatuma.
Alisema
kuwa baada ya tukio hilo waliamua kumpigia simu kijana huyo na ndipo alipokiri
na kueleza kuwa alifanya tukio hilo baada ya kupitiwa na shetani na kuomba
wamsamehe na kwamba hatorudia tena tukio kama hilo.
Hata
hivyo hawakuridhika na maelezo ya kijana huyo kutokana na kuelezwa na mtoto
huyo kwamba, tukio hilo halikuwa la kwanza
kutokea kwani amekuwa akimfanyika tendo hilo
mara kwa mara na mara nyingi humfanya majira ya usiku wakati mtoto
anapoenda kuosha vyombo.
Familia ya mtoto huyo iliamua kutoa taarifa polisi
baada ya kumweleza baba wa mtuhumiwa ambaye ni diwani wa kata ya mjini kati, na
kushindwa kuwapa ushirikiano ambapo walifika kituo cha polisi mjini kati na
kufungua
0 comments:
Post a Comment