NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akizungumza na
waandushi wa Habari, leo, katika Ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya
Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Picha na Bashir
Nkoromo
---
NA BASHIR NKOROMO,
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, baada ya kuutumia mwaka 2012 kupanga safu ya uongozi katika chaguzi za ngazi zote zilizomalizika hivi karibuni, mwaka ujao wa 2013 utakuwa wa kuchapa zaidi.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, baada ya kuutumia mwaka 2012 kupanga safu ya uongozi katika chaguzi za ngazi zote zilizomalizika hivi karibuni, mwaka ujao wa 2013 utakuwa wa kuchapa zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Naibu
Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba (pichani) alisema, kazi
itakayofanywa na CCM katika mwaka huo, ni pamoja na kukagua upya
utekelezaji wa ilani ya CCM na kuhakikisha zile ambazo hazikamilika
zinamalizwa.
"Mwaka huu wa 2012 unaomalizika tuliutumia zaidi kujipanga katika
uchaguzi wa ngazi zote ili kupata safu nzuri itakayoisimamia serikali
kutekeleza ilani ya CCM, sasa mwaka mpya wa 2013 utakuwa wa kazi zaidi
za kusimamia serikali ili kuhakikisha mwaka 2015 mpiganaji wa CCM
tutakayemteua kugombea urais anapita kiulaini", alisema Mwigulu.
Akizungumzia tukio la Mbunge wa Arusha Godless Lema kushinda
rufani yake dhidi ya hukumu iliyomvua ubunge Aprili mwaka huu, Mwigulu
alisema, ushindi huo ni ushahidi kwamba serikali ya CCM inaongoza kwa
misingi ya utawala bora ambapo kila anayestahili haki anapata.
"Ushindi huu wa Lema, siyo kwamba anaakili sana au chama chake
kina maarifa sana yaliyosababisha ushindi, ila ni kutokana na serikali
ya CCM iliyopo madarakani kuheshimu na kujali haki na kwa kweli natumia
fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuthamini na kusimamia haki wakati
wote.. Ninyi si mnajua katika nchi zisizo na utawala bora jinsi ambavyo
mambo huwa kwenye kesi kama hizi. lakini hapa Tanzania ni tofauti
kabisa", alisema, Mwigulu.
Aliwashangaa Chadema akisema, "Hawa ni watu wa aina yao,
waliposhindwa katika kesi Arusha walisema Ikulu imeingilia na majaji
hawajui kiingereza.. sasa leo wameshinda wanafurahi na kuona kwamba sasa
majaji wanajua kiingereza na hawakuigusa Ikulu kwamba imeingilia, maana
pale ilipotolewa hukumu umbali wake ni hatua chache na Ofisi ya Ikulu
kuliko Arusha".
Mwigulu alitumia fursa hiyo kuwatakia heri Watanzania kwa sikukuu za
Krismas na mwaka mpya na kuwataka kuzitumia sikukuu hizo kwa makini na
kwa kiasi ili zisiwe chanzo cha matatizo kwao badala ya furaha.
"Chama Cha Mapinduzi kinawatakieni sikukuu njema za Krismas na
mwaka mpya, lakini tunawaomba msherehekee kwa kiasi huku mkichunga
usalama wenu na mali zetu", alisema Mwigulu
0 comments:
Post a Comment