Rais
Barrack Obama wa Marekani ametoa wito kwa rais wa Rwanda Paul Kagame,
kusitisha msaada anaotoa kwa makundi ya waasi nchini Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Kwa mujibu wa ikulu
ya White House, rais Obama alifanya mazungumzo ya simu ya Rais Paul
Kagame siku ya jumanne, ambapo aliafiki tangazo lake la kujitolea
katika harakati za kupatikana kwa amani katika Jamuhuri ya kidemokrasia
ya Congo.
Waasi wa M-23 wapo katika eneo
la mashariki mwa Congo licha ya kuwepo kwa wanajeshi wa kutunza amani
wa umoja wa mataifa katika eneo hilo.
Ripoti
ya hivi majuzi iliyochapishwa na Umoja wa Mataifa iliishutumu serikali
ya Rwanda kwa kutoa msaada kwa waasi hao wa Congo, madai ambayo
serikali ya Rwanda Imekanusha vikali
0 comments:
Post a Comment