John Bocco |
Na Mahmoud Zubeiry
AJABU na
kweli. Robert Ssentongo amepewa tuzo ya ufungaji wa Kombe la Kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge jana, wakati anazidiwa mabao na washambuliaji
wa Tanzania Bara, John Raphael Bocco na Mrisho Khalfan Ngassa, ambao kila mmoja
ana mabao matano.
Ssentongo
amemaliza mabao manne, lakini jana CECAFA ikampa tuzo hiyo na kuwaacha wengi
midomo wazi.
Uganda ilitwaa
Kombe la Chalenge jana kwa kuifunga Kenya mabao 2-1, ambayo yote Kenya
walijfunga jana kupitia kwa wachezaj wao Anthony Kimani na Joackins Atudo. Bao
la Kenya lilifungwa na Edwin Lavatsa.
Mbali na
Ngassa na Bocco kuongoza wakifuatiwa na Ssentongo, wengine waliokuwamo kwenye
kinyang’anyiro ni Brian Umony wa Uganda aliyemaliza na mabao matatu, sawa
Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Zanzibar, Suleiman Ndikumana na Chris Nduwarugira wa
Burundi.
Wachezaji
wenye mabao mawili kila mmoja ni Geoffrey Kizito wa Uganda, David Ochieng, Mike
Barasa, Clifton Miheso wa Kenya na Dadi Birori wa Rwanda.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
John Bocco Tanzania 5
Mrisho
Ngassa Tanzania 5
Robert
Ssentongo Uganda 4
Brian Umony Uganda 3
Khamis Mcha Zanzibar 3
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
Chris
Nduwarugira Burundi 3
Geoffrey
Kizito Uganda 2
David
Ochieng Kenya 2
Clifton
Miheso Kenya 2
Dadi Birori Rwanda 2
Mike Barasa Kenya 2
0 comments:
Post a Comment