Ngassa akibusu mpira jana |
Na Mahmoud Zubeiry,
Kampala
MSHAMBULIAJI
wa Tanzania Bara, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kwamba pamoja na kuongoza kwa
mabao katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker
Challenge lakini atafurahi hata kama mfungaji bora akiwa mchezaji mwenzake wa
Kilimanjaro Stars, John Bocco ‘Adebayor’.
Ngassa
anaongoza kwa mabao yake matano, aliyofunga katika mechi moja tu dihidi ya
Somalia jana, wakati Bocco ana mabao manne, aliyofunga mawili kila mechi dhidi
ya Sudan na jana na Wasomali.
Akizungumza
na BIN
ZUBEIRY baada ya mechi ya jana, Ngassa alisema kwamba yeye kama
mchezaji anaweka mbele maslahi ya timu hivyo mfungaji bora akiwa yeyote baina
yake na Bocco atafurahi.
“Siku zote mimi
napocheza huwa naweka mbele maslahi ya timu, ndiyo maana ukifuatilia rekodi
yangu kuanzia kwenye Ligi Kuu, mimi ndiye mchezaji ninayeongoza kutoa pasi za
mabao,”alisema Ngassa.
Jumla ya
mabao 44 hadi sasa yamefungwa katika mechi 24 za kwenye hatua ya makundi pekee
tangu kuanza kwa mashindano haya Novemba 24.
Wakati
Ngassa anaongoza kwa mabao yake matano, akifuatiwa na Bocco wa Azam FC mwenye
manne, nafasi ya tatu wanafungana Suleiman Ndikumana wa Burundi mwenye mabao
matatu, moja la penalti, Brian Umony wa Uganda na Chris Nduwarugira wa Burundi
pia.
Wanaofuatia
ni Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Zanzibar mwenye mabao mawili sawa na David Ochieng
na Clifton Miheso, wote wa Kenya.
Waliofunga
bao moja kila mmoja katika mashindano haya ni Yussuf Ndikumana wa Burundi, Mohamed
Jabril wa Somalia kwa penalti, Geoffrey Kizito, Hamisi Kiiza, Robert Ssentongo
wote wa Uganda Yonatal Teklemariam wa Ethiopia, Haruna Niyonzima, Jean
Mugiraneza, Dadi Birori, Tadi Etikiama na Tumaine Ntamuhanga, wote wa Rwanda.
Wengine
wenye bao moja kila mmoja ni Ramadhan Salim wa Kenya, Gatech Panom Yietch wa
Ethiopia, Farid Mohamed wa Sudan, Chiukepo Msowoya, Miciam Mhone, Patrick
Masanjala, wote wa Malawi, Amir Hamad Omary na Yosief Ghide kwa penalti, wote
wa Eritrea.
WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE
2012
Mrisho
Ngassa Tanzania 5
John Bocco Tanzania 4
Suleiman
Ndikumana Burundi 3 (1 penalti)
Brian Umony Uganda 3
Chris
Nduwarugira Burundi 3
Khamis Mcha Zanzibar 2
David
Ochieng Kenya 2
Clifton
Miheso Kenya 2
Yussuf
Ndikumana Burundi 1
Mohamed
Jabril Somalia 1(penalti).
Geoffrey
Kizito Uganda 1
Hamisi Kiiza Uganda 1
Robert
Ssentongo Uganda 1
Yonatal
Teklemariam Ethiopia 1
Haruna
Niyonzima Rwanda 1
Jean
Mugiraneza Rwanda 1
Dadi Birori Rwanda 1
Tadi
Etikiama Rwanda 1
Tumaine
Ntamuhanga Rwanda 1
Ramadhan
Salim Kenya 1
Gatech Panom
Yietch Ethiopia 1
Farid
Mohamed Sudan 1
Chiukepo
Msowoya Malawi 1
Miciam Mhone
Malawi 1
Patrick
Masanjala Malawi 1
Amir Hamad
Omary Eritrea 1
Yosief Ghide
Eritrea 1(penalti).
0 comments:
Post a Comment