.

.
Sunday, December 2, 2012

2:14 PM
Na Bertha Ismail- Longido

Baraza la madiwani  wilayani Longido limelezea kukerwa na urasimu uliopo hivi sasa katika wizara ya afya na ustawi wa jamii kukwamisha ufunguzi  wa zahanati mbalimbali zilizojengwa na wananchi wilayani humo
Hali hii imelezewa kuwakera zaidi madiwani wote katika halmashauri hiyo  ya kukwamisha huduma za  afya  katika wilaya hiyo na kuwa chanzo cha  wazazi na watoto wadogo wengi kupoteza maisha
Katika kikao cha siku moja kilichofanyika wilayani Longido hivi karibuni chini ya  Mwenyekiti   Joseph Sadira, wajumbe  wa baraza hilo la madiwani  wameshutumu vikali hatua ya wizara hiyo kushindwa kutoa kibali kwa ajili ya kufungua zahanati ya kijiji cha Ilorienite iliyoko katika kata ya  Ilorienite tarafa ya Ketumbeine  wilayani humo kwa zaidi ya miaka minne hadi sasa
 
Diwani  Bibi  Sion  Kereine  wa Kitumbeine  akielezea kwa masikitiko katika kikao hicho  amesema wajawazito  na watoto wachanga wamekuwa wakipoteza maisha kila mwezi kutokana na kukosa huduma huku serikali ikiendeleza urasimu usio na tija wala manufaa kwao.
Bibi  Kereine alisema kuwa serikali imeshindwa kufungua zahanati hiyo tangu ilipojengwa  kwa nguvu za wananchi mwaka 2006 ikiwa imekamilika kila kitu  zikiwemo nyumba za watumishi  na vyoo pamoja na baadhi ya wafadhili kutoka nje kuipatia vifaa vyote muhimu katika uendeshaji wa  huduma za afya.
 
Bibi Sion Kereine  ametoa mfano  wazazi  wapatao sita na watoto wachanga  11 hupoteza maisha kutokana na kukosa  huduma ya zahanati hivi karibuni wilayani humo huku viongozi waliopo wakishindwa kutoa ufafanuzi wa kujitosheleza juu ya ufunguzi wa zahanati hiyo.



Aidha zahanati hiyo haina watumishi  na pia haipati mgao wa dawa kutoka wizara ya afya  hata kama  watumishi wangekuwepo kutokana na kutotambuliwa na serikali. Ameeleza diwani huyo bi Sion
Hivi sasa   wananchi hao wanalazimika kusafiri umbali wa kilomita kati ya 28 na 30 kufuata huduma  Ketumbeine ama  Engaruka umbali wa   kilomita 40  kwa kuwabeba wagonjwa katika machela  ama punda. Ameeleza  mwana mama huyo diwani wa  Ketumbeine
Kijiji hicho chenye vitongoji sita  kina zaidi ya watu  10,000  wanaohitaji huduma ya afya kutoka katika zahanati hiyo.amemwomba Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuingilia kati  suala hili haraka  ili kunusuru  maisha ya wananchi katika kijiji hicho
Wilaya ya Longido hivi sasa ina zahanati 20 kati ya hizo  zahanati nne hazifanyi kazi kutokaa na  tatizo la  urasimu   wa kuzifungua  pia kuna vituo vya afya   vitatu

baadhi ya madiwani wakichangia jadala kuhusu uduma za afya wilayani humo wammtaka mganga mkuu wa wilaya  hiyo kufuatilia kwa karibu utendaji wa watumishi    wa idara hiyo katika zahanati  zote kwani utendaji wao wa kazi hauridhishi wala kukidhi haja wa wagonjwa kutokana na wizi wa dawa.

Walidai kuwa baadhi ya watumishi hao  wamefungua maduka ya ya dawa  ambako ndiko dawa zinazopelekwa zinazotolewa na  serikali ambapo huelekezwa huko ili kuwauzia wananchi kwa bei ya juu laa sivyo wagonjwa wataishia kupima bila kupewa dawa wala kutibiwa.
akizngumza  katika kikao hicho mwenyekiti wa baraza la madiwani  bwana joseph  alisema wagonjwa wengi wanakosa kupata dawa katika zahanati za serikali kutokana na kuletwa chache na badala yake  wanalazimika  kununua katika  maduka ya dawa yaliyofuguliwa na watumishi hao
amesisiza kuwa  dawa  nyingi zinazoletwa  na  serikali zinakua katika maduka ya watumishi wa  idara ya afya  wanaofanya kazi    katika zahanati hizo za vijijini hivyo kupelekea vituo hivyo kukosa dawa.
Akizungumza katika kikao hicho cha baraza la madiwani mganga mkuu wa wilaya Dkt  Jonathan Budenu  kuhusiana na madai hayo  hususani zaahanati hiyo kushindwa kufunguliwa  amesema  imetokana na  ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa arusha kushindwa kufanya ukaguzi badala yake hukaa ofisini kusubiri ripoti tuu.
Aidha  amewambia madiwani hao kuwa wilaya hiyo inapata mgao mdogo  wa dawa   kutokana  na takwimu ndogo ya mwaka 2002 inayotumika hadi sasa ambayo inaonyesha idadi ndogo za watu waliopo wilayani humo ambao ni 96,000 kwa mujibu  wa takwimu hizo za mwaka 2002.
Ametoa mfano mwaka huu wizara ya afya imeipatia halmashauri hiyo kiasi cha shilingi milioni 68 tu kwa ajili ya ununuzi wa dawa kiasi ambacho ni kidogo ikizingatiwa na idadi ya wananchi walioko wilayani humo.

0 comments:

Post a Comment