KATIKA hali isiyokuwa ya awaida Mwanamke mmoja aliyefahamika
kwa jina la Neema Teti ambaye pia ni mwalimu,mkazi wa Shangarai mkoa wa Arusha
amepata majeraha makubwa sana
mara baada ya kumwagiwa maji ya moto sehemu zote za mwili wake mara baada ya
kuhofiwa kuwa anatembea na mume wa mtu
Aidha tukio hilo
lilitokea December tisa majira ya asubuhi katika eneo la Shangarai ambapo Bi Neema alimwagiwa maji ya moto na rafiki
yake kwa kuhofiwa kuwa anatembea na mume wake
Akiongea na waandishi wa habari mapema jana katika hospitali ya Mt Meru
ambapo anapatiwa matibabu Bi Neema alisema kuwa siku hiyo ya December tisa
rafiki yake ambaye bi Tatu Msuya alienda
nyumbani kwake na kumuomba kuwa waweze kwenda kwa pamoja kwani kuna matatizo na
hivyo yeye ndio anatakiwa kusimamia familia yake.
Neema alidai kuwa mara baada ya kufika nyumbani kwa rafiki yake
kwa malengo ya kumsaidia shida aliyonayo
ambayo alidai ni msiba lakini walipofika mambo hayakuwa hivyo
Aliongeza kuwa mara baaada ya hapo rafiki yake ambaye ni Bi
Tatu alimtaka aingie ndani ili waweze kupanga mambo yao
ya jinsi ya kusaidia familia kwa kipindi hicho cha msiba jambo ambalo hakuwa na
wasiwasi nalo kwa kuwa walikuwa wanaaminiana sana
“baada ya hapo nilishangaa sana kwani alifunga milango yote na kuongeza
makofuli jambo ambalo halikunipa shida kwa haraka kwani niliwaza labada anataka
mazungumzo yawe siri”aliongeza Neema
Alidai kuwa mara baada ya tukio hilo
la kufungwa milango,yote ya nyumba ya rafiki yake ndipo alipomtaka aweze kunywa
soda lakini alikataa kwani ilikuwa ni asubui sana
lakini pia soda hiyo ilikuwa na chupa ndogondogo jambo ambalo halikuwa
na ishara nzuri
“nilishangaa kwa kuwa aliniletea soda ambayo ilikuwa na
chupa ndogondogo ndani lakini nilijiuliza kwanini huyu rafiki yangu
ananilazimisha zaidi ninywe soda asubui na inaonekana inasumu machale
yalinicheza lakini sikuweza kutoka kwa kuwa alikuwa tayari ameshafunga milango
yote huku baadhi ya watu wa familia yake nao wakiwa wamefungiwa ndani”aliongeza
zaidi Neema
Pia alidai baaada ya muda
mfupi rafiki yake alikuja na maji ya moto ambayo yamechemka sana na kuanza kumwagia
bila kujali kuwa ni rafiki yake jambo ambalo pia lilifanya ashindwe kupata
msaada wa haraka kwa kuwa milango yote alikuwa ameifunga
“alinimwagia maji ya moto kama
kuku bila hata kunionea huruma huku akidai kuwa analipiza kwa kuwa ameambiwa
mimi natembea na mume wake na nina mimba ya mume wake jambo ambalo sio kweli na
alidai anachotaka ni kunitoa roho”aliongeza Neema
Alidai kuwa baada ya tukio hilo
alifungua mkilango na kisha kuchukua mizigo yake haraka na kisha kukimbia
kusikojulikana jambo nalo liliwafanya majirani wa eneo hilo kuweza kukusanyika na kisha kumpa msaada
wa kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa lakini pia kumfikisha
hospitalini
Awali Muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo ya Mte Mt Meru ambaye ni Bi Neema Baya alisema kuwa hali ya mgonjwa
huyo inaendelea vizuri japokuwa bado ana maumivu makali na pia ametoa wito kwa wanawake
wengine kuacha tabia ya ukatili kama hiyo kwani
inaweza kusababisha vifo.
Wakati huohuo Jeshi la polisi mkoa wa Arusha kupitia Kitengo
cha dawati la jinsia limedai kuwa bado linamtafuta Bi Tatu kwa kosa ambalo amelifanya
kwani tukio hilo
ni la kinyama na nitukio ambalo halipaswi kutokea tena kwenye jamii
Akiongea kwa niaba ya Jeshi hilo
Maria alisema kuwa kwa kuwa jeshi hilo lina
mkono mrefu basi litahakikisha kuwa linamtafuta Bi tatu na kisha kumfikisha mahakamani
kwa kuwa amefanya kitendo kibaya sana
kwa mwenzake baada ya kumuhisi kuwa anamahusiano ya kimapenzi na Mume wake.
0 comments:
Post a Comment