makundi mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli hii leo |
Katibu wa
Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro (TLB), Protas Soka Akisoma risala kwa niaba ya makundi hayo mbele ya mbunge wa jimbo la monduli
Viongozi
mbalimbali wa makundi ya kijamii wakiwa wanamkabidhi waziri mstaafu
ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowasa bahasha yenye
fedha taslimu shilingi milioni mbili laki tano sitini na saba elfu na
mia sita zilizochagwa na wananchi kwa ajili ya kwenda kuchukuwa fomu
ya kugombea nafasi ya Urais
mbunge
wa jimbo la monduli akiangalia picha ambayo ametengenezewa na vijana
kutoka makundi wakati walipomtembelea nyumbani kwake monduli kwa ajili
ya kumkabidhi fedha kidogo kwa ajili ya kuchukuwa fomu ya kugombea urais
makundi
mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya
Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli hii leo
makundi
mbalimbali ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya
Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Manyara wakiwa wanaandamana kwa pamoja kuelekea kwa mbunge wa jimbo la monduli hii leo
Mratibu
wa Marafiki wa Lowasa Kanda ya Kaskazini, Noel
Nnko,akiwa anamuonyesha picha ambayo ni ya kumbukumbu ya tukio la leo la
kuja kumuunga mkono mbunge wa jimbo la monduli pamoja na kumuomba
atangaze nia ya kugombea nafasi ya urais
maandamano ya pikipiki yakiwa yanaelekea nyumbani kwa mbunge wa jimbo la monduli hii leo
Wananachi zaidi ya 700 kutoka makundi mbalimbali
ya kijamii ya mikoa ya Kaskazini, inayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Tanga,
Arusha na Manyara, wamejitokeza nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Monduli (CCM), Edward Lowasa, wakimshawishi atangaze nia ya kugombea urais kupitia
chama hicho.
Wananchi
hao kutoka katika Makundi mbalimbali katika
ya mikoa hiyo yamewasili leo
nyumbani kwake,Kijiji cha Ngarashi, Wilaya ya Monduli baada ya kufanya
maandamano makubwa yaliyoanzia njia panda ya Monduli, wakiimba nyimbo za
matumaini kwamba ‘wewe ni tumaini la walio wengi Tanzania, maamuzi na matumaini
mapya, watanzania wako nyuma yako’.
Aidha
akisoma risala kwa niaba ya makundi hayo baada ya kuwasili nyumbani hapo ,
Katibu wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Kilimanjaro (TLB), Protas Soka
alisema kwa nia thabiti isiyo na kigugumizi asilani, wanaharakati hao pamoja na
watanzania wengine wanamhitaji (Lowasa) kwa unyenyekevu na hivyo,
wanamwomba atangaze nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais mwaka 2015.
“Leo
watanzania tumepaza sauti zetu kwa pamoja kuanzia ngazi ya
Kaya,Kitongoji,Kijiji,Kata, Tarafa,Wilaya, Kanda mpaka Taifa wakisema Viva
Lowasa, Tobiko Lowasa. Kwa moyo mmoja bila kushawishiwa na mtu wala kikundi
chochote; wanaharakati hawa wamekuona wewe, mheshimiwa Edward Lowasa ndio
kiongozi sahihi kwa mustakabali na manufaa ya taifa letu,”alisema Soka
Makundi
hayo ambayo ni walemavu, waendesha bodaboda, walimu, wataalam wa afya, vijana
na wanasiasa, walimchangia Lowasa kiasi cha shilingi milioni 2,567,600 kwa
ajili ya kununua au kulipia fomu ya kugombea nafasi ya Urais pindi
atakapotangaza nia.
“Kwa
lugha nyingine sasa tunakuomba Mheshimiwa Lowasa sasa tunakuomba utangaze nia
ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,”alisema Soka.
Makundi
hayo yaliyoongozwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) mkoa wa Kilimanjaro, Paul Matemu, Mratibu wa Marafiki wa Lowasa Kanda ya
Kaskazini, Noel Nnko,Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Umoja wa Vijana (UVCCM), mkoa wa Arusha, Robnson Meitinyiku, Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa Taifa, Fred Mushi, Askofu wa Kanisa la Calvary Assemblies of
God, Christoher Madilu ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa na Abdalah
Sadick kutoka mkoa wa Manyara.
Akizungumza
mara baada ya kupokea makundi hayo mbunge huyo wa jimbo la monduli alisema kuwa
amekubaliana nao na anatarajia kutangaza rasmi nia mwezi aprili pindi tu chama
chake kitakapo ruhusu
“Nitatangaza nia mwezi Aprili mwaka huu, pale
uwanja wa Shekhe Amri Abeid mjini Arusha baada ya chama changu kupuliza
kipenga. Ninachowaomba watanzania kwa sasa, mniombee katika safari yangu ya
matumaini,”alisema Lowasa.
0 comments:
Post a Comment