Mwenyekiti
wa tawi la yanga Arusha, Richard Elibariki Mollel amesema kuwa utafiti
uliofanywa na wanachama wa yanga ikiwemo tawi la Arusha umeonyesha kuwa tangu
yanga ianze kusajili wachezaji kutoka simba au waliowahi kuchezea samba timu
yao ya yanga imekuwa ikifungwa na simba na shutuma kuangukia wachezaji hao.
Hivi sasa
yanga inawachezaji zaidi ya watano tena wa kikosi cha kwanza waliowahi
kuichezea simba na ukiangalia ndio chanzo cha yanga kugeuka vibonde kwa simba
kikiwemo kipigo cha wiki iliyopita cha bao 1-0 na safari hii lawama zikiwaangukia
Danny Mrwanda na kipa Alli Mustafa ‘Bartez’.
Mshabiki
mkubwa wa timu ya Yanga mkoani hapa Ernest Manyilizu alisema kuwa tunaomba
uongozi kama watatusikia warudie mfumo wa zamani wa kuwasajili wachezaji wakali
kutoka timu zingine za mikoani kuliko kuelekeza macho yao kwa mkoa wa
Dar-es-salaam hali ambayo inatutia aibu kufungwa na timu Simba kila mara kwa
sisi kuwa vibonde wao.
“Mimi niseme
tu kuwa uongozi wa juu wa Yanya utupe mahitaji yetu sisi mashabiki wao kwa
kuachana na kusajili wachezaji waliowahi kutumika Simba kwani inawezekana
wachezaji hao wakaja na mapenzi ya Simba kuitumikia Yanga hivyo ni rahisi
kufanya urafiki wa kuwaachia ushindi na kama unavyojua ni bora kufungwa na timu
zingine kuliko tufungwe na Simba hii ni aibu sana kutokana na sisi mbali na
kuwa wakongwe wa soka lakini kumbuka ni watani wa jadi” alisema Ernest
Manyilizu.
Mwanachama
mwingine wa yanga Kefasi Filex “Sunguti” anasema “hata enzi za akina Nuruduni Bakari,
Juma Kaseja na Athuman Idd Chuji, yanga
imekuwa ikifungwa kirahisi na wana Simba na sasa suluhisho ni kutema wachezaji
wote waliowahi kuchezea Simba na kuepuka kusajili wachezaji toka kwa wapinzani
wetu hao wa jadi, hivyo waangalie mpango mwingine wa kupata wachezaji wazuri
ikiwemo hata kufanya mashindano maalum ya kusaka wachezaji au kutafuta nyota
wakali katika timu hizi ndogo”
Mwisho………………………………..
0 comments:
Post a Comment