na Bertha Ismail - Arusha
Viongozi wa
zamani wa chama cha soka wilayani Arusha ADFA wanajipanga upya kuingia madarakani
katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika wakati wowote kuanzia sasa kufuatia
uongozi uliopo madarakani kumaliza muda wake.
Viongozi hao
wakiongozwa na katibu wa zamani wa ADFA Robert Munis wamekuwa wakifanya vikao
vya kupanga mikakati madhubuti wa kuwang,oa madarakani kamati yote ya utendaji
ya ADFA kwa kigezo cha kuporomosha soka la Arusha kwa kuvipa vilabu mzigo wa
michango mbali mbali ikiwemo ada kubwa ya ushiriki ligi hali ambayo timu nyingi
zenye uwezo zimekwama kushiriki ligi za taifa kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa.
Hadi sasa
vikao zaidi ya vinne vimeshafanyika katika mgahawa maafuru unaojulikana kama
Spice Inn uliopo pembezoni mwa uwanja wa Sheih Amri Abeid na kushirikisha
wajumbe wa zamani wa ADFA akiwemo Hessein Lembarity aliyekuwa mwenyekiti, Abdul
kondo aliyekuwa mjumbe na mkurugenzi wa rollingstone Ally Mtumwa aliyewahi kuwa
mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF.
Akizungumzia
lengo lao hilo la kurudi kwenye uongozi, Robert Munis anasema yeye alistaafu
kwa hiyari yake baada ya kuwa katibu kwa zaidi ya miaka 10 kutokana na kuzidiwa
na maswala na kazi na familia huku akiamini atakaowaachia wataendeleza mema
yale ikiwemo kuziongeza timu nyingi kushiriki ligi mbali mbali sambamba na
kubuni mashindano mengine mengi kuongeza idadi ya yaliyokuwepo lakini hali
haikuwa hivyo.
“Unajua mimi
nilizidiwa na maswala yangu ya kazi na familia hivyo nikabidi niachie ngazi
moja nishikilie familia na kazi yangu huku nikiamini hawa nitakaowaacha
watafanya muendelezo lakini nasikitika sana kusikia eti soka la Arusha sasa
limedorora na mashindano mengi yaliyokuwepo yamekufa hali ambayo ni mbaya sana
timu kufanya mazoezi pekee kwa ajili ya ligi ya Taifa”
“Hivyo basi
kama mdau wa soka mkoa huu sitakubali kuona soka la Arusha linakufa kifo cha
aibu kiasi hiki kutokana na uzembe ulioko madarakani ni bora tuwaondoe turudi
tufanye kazi na niombe wadau wa Arusha wajitokeze kuunga mkono hili lifanikiwe
kurudisha heshima ya Arusha kuwakilishwa na timu mbili hadi taty ligi za juu
(daraja la kwanza na ligi kuu)” alisema Robert alieonekana wazi kujaa jazba.
Alisema kuwa sasa analazimika kurejea kwa
kishindo baada ya kusikitishwa na kuporomika kwa soka la Arusha na kutengwa kwa
soka la Arusha na wadau mbalimbali wakiwemo wafadhili, wafanyabiasha na viongozi
wa kitaifa ambapo alisema kuwa chanzo cha kudorora kwa soka.
Inasikitisha
mkoa wa Arusha uliowahi kuwa na timu tatu ligi kuu sasa hakuna hata timu moja
na hata michezo ya kimataifa iliyokuwa ikichezwa Arusha sasa haichezwi achilia
mbali kuharibika kwa uwanja wa sheikh Amri Abeid kutokana na kujaa mashimo kila
upande huku vichuguu vikichipuka kila pembe na majani yake kunyauka kutokana na
viongozi wa soka kufumbia macho swala hili, huku viwanja vingine tegemezi
vikifungwa bila uongozi kuomba upendelea kwa timu kufanyia ,mazoezi na
mashindano.
Aidha
uchaguzi wa soka ngazi za wilaya za mkoa wa Arusha zinatarajiwa kuanza wakati
wowote kuanzia mwezi Aprili huku wagombea wa nafasi mbali mbali wakipigana vijembe
chini chini kuwania nafasi hizo lakini wengi wao wakitupia lawama uongozi wa
sasa na kuwa na nia moja ya kuwang’oa madarakani.
Mwisho……………………..
0 comments:
Post a Comment