|
MKUU
wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, leo ameongoza mamia ya wakazi wa
Jiji la Mwanza na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa kumuuaga mwili wa
marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu ‘Marsh’,yaliyofanyika uwanja wa Shule ya msingi Mirongo Jijini Mwanza. |
|
Meya
wa Jiji la Mwanza , Stanslaus Mabula alisema,jiji la Mwanza akielezea
wasifu wa marehemu Marsh, ikimbukwe kuwa Mstahiki ndiye mlezi wa kituo
cha soka cha Marsh Academy. |
|
Mchezaji
wa zamani wa Yanga na Timu ya Taifa Stars, Edibily Jonas Lunyamila
(kushoto) akielezea alivyomfahamu marehemu Marsh, na kulia ni mchezaji
wa zamani wa timu ya Pamba, Yanga na Taifa Stars. Fumo Felician akiwa na
majonzi. |
|
Msanii wa tasnia ya filamu nchini Steve Nyerere akitoa ushuhuda wake. |
|
Katibu
wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akitoa salamu za rambirambi na
kuelezea jinsi Marsh alivyokuwa mwaminifu na kuwa mwanachama hai hata
kwenye nyanja za siasa, wengine ni makatibu wa chama hicho toka wilaya
mbalimbali mkoani Mwanza. |
|
Familia. |
|
Viongozi na wadau wa soka. |
|
Hassan kiraka akiwa amemshika mkono kumuongoza mmoja ya watoto wa kituo cha Marsh Academy. |
|
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya H.Baba akitoa heshima zake za mwisho. |
|
Safu ya viongozi ni huzuni tupu.... |
|
Nini hatma ya vijana hawa wa kituo cha soka cha Marsh Academy. |
|
Huzuni kwa timu ya U17 toka kituo cha Marsh Academy. |
|
Sehemu ya umma uliofika eneo la tukio. |
|
Sehemu ya umati uliwakilisha makaburini. |
MKUU wa Mkoa wa Mwanza,
Magesa Mulongo, leo ameongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa
jirani ya Kanda ya Ziwa kumuuaga mwili wa marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu ‘Marsh’,yaliyofanyika kwenye makaburi ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza.
Pia katika mazishi hayo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, aliwaongoza waombolezaji katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na viongozi wa serikali na vyama
vya siasa, madhehebu ya dini,wananchi, wadau wa michezo,wanasoka wa
vizazi mbalimbali ,makocha na waamuzi kutoka mikoa mbalimbali nchini.
Mulongo
aliwaasa waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa kocha huyo kwenye
uwanja wa shule ya Msingi Mirongo kuwa ,ili kumuenzi kwa vitendo ,wadau
wa soka mkoani hapa wachague timu moja na uwanja utakaoitwa jina lake.
Mkuu
huyo wa mkoa wa Mwanza, aliutaka uongozi wa chama cha Soka mkoa wa
Mwanza (MZFA) waandae programu ya kuanzisha michuano ya mpira wa miguu
itakayofanyika kila mwaka na kuiwasilisha ofisini kwake ikiwa na lengo
la kumuenzi kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji vya vijana na
kuviendeleza kama ilivyokuwa dhamira ya marehemu.
Aidha
Mgeja akimzungumzia marehemu alisema marehemu Marsh aliwea kujitolea
kuitangaza Mikoa Mara, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Dar es salaam na taifa
katika medani ya kimataifa,wakati akifundisha vilabu mbalimbali vya
hapa nchini ikiwemo timu za taifa ya vijana Serengeti boys na Taifa
stars.
Kwa
wake Meya wa Jiji la Mwanza , Stanslaus Mabula alisema,jiji la Mwanza
litatenga viwanja vya michezo kwa ajili ya kuibua vipaji vya vijana
wadogo wa lika tofauti zaidi ya 200 kwa nyakati tofauti na ambao
marehemu alikuwa akiwahangaikia kuwalea kwa maisha ya soka katika maisha ya uhai wake.
“Amekuwa
mwanzilishi wa vitalu vya kuendeleza mchezo wa soka mkoani na nchini
hapa,matunda yake yameonekana kwa kutoa vijana wenye uwezo ambao
wameweza kutoka nje kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa
lakini pia wapo wanaocheza katika vilabu vya Ligi Kuu nchini,”alisema Mabula.
Wadau
mbalimbali wa soka wakiwemo wachezaji wa zamani na wa kizazi cha sasa,
walionesha masikitiko yao makubwa kwa kumpoteza mtu muhimu katika
familia ya soka,kwamba pengo lake haliwezi kuzibika kutokana na mchango
wake wa kuendeleza mpira wa miguu nchini katika maeneo aliyofanyia kazi
ya ukocha.
Diwani
wa Kata ya Mirongo Daudi Mkama (CUF) alimpongeza Meya wa Jiji la Mwanza
Mabula kwa moyo wake wa kujitolea na kuamua kugharamia sehemu kubwa ya
mazishi ya marehemu Marsh tangu kuwasili kwake, kuagwa na kupelekwa
nyumbani kwao Igoma na wananchi wa maeneo hayo kutoa heshima za mwisho
kabla ya kushiriki mazishi yake yaliyofanyika makaburi ya Igoma nje
kidogo ya Jiji la Mwanza.
"Munyonge
munyongeni na mtu anayefanya jambo jema hatuna budi kumsifia na
kumpongeza, kwa hili alilolifanya Mstahiki meya wa Jiji, Mabula la
kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa kwa asilimia 90 ni kuonyesha
ameguswa lakini kama kiongozi wa watu ametekeleza wajibu wake kwa moyo
wake wa kujitolea,"alisisitiza Mkama.
Wadau
wa soka kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiongozwa na RC Mulongo, Meya
Mabula, DC Baraka Konisaga (Nyamagana), DC Angelina Mabula (Iringa),
Kocha na Mwakirishi wa TFF Salum Madadi, Mwenyekiti wa MZFA Jackison
Songola, Mbunge wa Jimbo la Rorya - Mara Lameck Airo (CCM) kumuaga na
kisha mazishi yake kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga
Khamis Mgeja, wananchi na wadau wengine.
0 comments:
Post a Comment