kamanda Liberatus Sabas |
na Bertha Ismail - Arusha
Jeshi la
polisi mkoani Arusha limewataka wakazi wa Arusha kujitokeza kuutambua mwili wa
mwanamke mmoja mwenye umri kati ya miaka 18-20 aliyekutwa amefariki huko eneo
la mjini kati jirani na ofisi ya CCM mkoa.
Akizungumza
na gazeti hili, kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, kamanda Liberatus Sabas
alisema kuwa mwili huo uliohifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika
Hospitali ya mkoa, Mount Meru umeokotwa mapema jumatatu march 23 mwaka huu
ndani ya Carvati liliopo eneo la CCM mkoa.
Alisema
mwili wa mwanamke huyo bado haujatambuliwa
hadi sasa jina wala makazi yake ambapo inasadikika marehem alifariki na
kukaa hapo zaidi ya wiki moja huku chanzo cha kifo kikiwa hakijafahamika hadi
sasa ambapo mwili huo umegundulika kutokana na harufu kali iliyokuwa inatoka
kwenye eneo hilo.
“Baada ya
watu kusikia harufu hiyo ndio kuchunguzwa inapotokea na kubainika kuwepo kwa
mwili huo ulioanza kuoza na jeshi la polisi kwa kushirikiana na zima moto
walifanikiwa kuutoa na kuuhifadhi mount meru.
Wakati huo
huo jeshi la polisi limefanikiwa kukamata magunia 11 ya madawa ya kulevya aina
ya bhangi na mtu mmoja aliyekuwa akisafirisha huko maeneo ya bara bara ya
Arusha / Namanga wilayani Longido mkoani Arusha.
Akizungumza
na waandishi, Kamanda Sabas alisema kuwa madawa hayo yalikuwa yakisafirishwa kutoka
Arusha kuelekea Longido kupitia gari Toyota land Crusa Pick-up yenye namba T.695
ARR Mali ya kampuni ya uwindaji ya Wengert Windrose iliyokuwa ikiendeshwa na
Frank Faustine (40).
“Kufuatia
tukio hilo, pia tunamshikilia dereva huyo Frank Faustine kwa upelelezi zaidi na
akibainika kuhusika sheria itachukua mkondo wake, ila naomba kutoa wito kwa
wakazi wa Arusha kuacha kujishughulisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya
na wafanye biashara halali ya kujipatia kipato” alisema Sabas
Mwisho……………….
0 comments:
Post a Comment