VITA YA KUPAMBANA NA UJANGILI YASHIKA KASI,KIKOSI CHA KUPAMBANA NA UJANGILI CHAPATA SILAHA ZA KISASA
Arusha.Kikosi
cha kupambana na ujangili nchini kimepata vitendea kazi kutoka kwa
wadau wa sekta ya utalii vitakavyowezesha kukabiliana na matukio ya
ujangili yaliyoshika kasi nchini na kuhatarisha kutoweka baadhi ya
wanyama.
Miongoni
mwa misaada iliyotolewa ni magari matano aina ya Land Cruser yenye
thamani ya Sh 750 milioni,bunduki za kivita 50 aina ya Ak 47 na risasi
10,000 na Magazini 20 ambazo thamani haikutajwa kwa kwasababu za
kiusalama.
Waziri
wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu baada ya kukagua vitendea kazi
hivyo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)
amesema vitasaidia kuongeza nguvu za kufanya doria na kupambana na
ujangili kwenye mapori ya akiba nchini na kudhibiti utoroshwaji wa nyara
za serikali.
Nyalandu
amekiri kuwapo kwa changamoto ya mwingiliano wa maeneo yaliyohifadhiwa
na makazi ya wananchi ambayo inatatuliwa kwa mujibu wa ilani ya
uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)lengo likiwa kuwa na uhifadhi
endelevu ambao unaleta maendeleo endelevu kwa wananchi.
Naye
Naibu Mkuu wa Kikosi cha kupambana Ujangili Kanda ya Kaskazini,Michael
Msuka amesema vitendea kazi hivyo vitaongeza hari ya watumishi katika
kulinda wanyamapori katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Manyara na Tanga.
Alisema
vita ya kupambana na ujangili ni kubwa kwani katika kipindi cha mwezi
Septemba hadi Disemba mwaka 2014 jumla ya majangili 203 walikamatwa
kwenye maeneo mbalimbali nchini na kuwa wamefikishwa mahakamani na
baadhi yao kutozwa faini.
0 comments:
Post a Comment