Wadau wa
michezo mkoani Arusha wamemtaka Naibu Waziri wa Vijana Utamaduni na Michezo
atembelee na kukagua uwanja wa Sheikh Amri Abeid ajionee jinsi ulivyo katika
hali mbaya kiasi cha kutokuwa katika hadhi ya kuchezewa hata mashindano ya
mchangani.
Kauli ya
wadau imekuja baada ya Naibu Waziri Juma Mkamia kutoa kauli kuwa uwanja wa Sheikh
Amri Abeid ni katika viwanja bora vinavyotambulika na shirikisho la mpira
Afrika (CAF) na unaweza kutumika na michezo ya kimataifa, kauli iliyopingwa
vikali.
Viongozi wa
vilabu, wachezaji na hata wadau wa soka wameshangazwa na kauli ya Mkamia na
kuonyesha wasiwasi kuwa Waziri huyo hajawahi kuutembelea na kuujuwa vema uwanja
huo kwa
kuukagua uwanja na miundo mbinu yake.
Eliapenda
Zambia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya michezo ya TACODA alisema kuwa hali ya
uwanja ni mbaya mno kiasi kwamba ni bora kucheza katika viwanja vya mchangani
kuliko uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliotawaliwa na mashimo, vichuguu, milima na
mabonde huku vyoo vikiwa tatizo.
Juu ya
miundombinu ya uwanja huo pamoja na uwepo na maji ya kutosha lakini hakuna vyoo
vya watazamaji na vya wachezaji vikiwa vichafu na kuweka hali ya ukungu huku
baadhi ya vyumba vya choo vikigeuzwa maduka na kupangisha wafanyabiashara na
kuwa sehemu ya mapato ya CCM wenye uwanja.
Aidha suala
hilo liliwahi kupigiwa kelele na wasimamizi wa vituo vya ligi ya Vodacom, Daraja la kwanza na viongozi
wa chama cha mpira mkoa (ARFA) juu ya kurekebisha vyumba vya kuvalia wachezaji
pamoja na vyoo kuweka marumaru na madirisha lakini jitihada hizo hazijazaa
matunda mpaka sasa huku nyasi zikikauka kabisa na kujenga hali ya viraka.
Waziri Juma
Mkamia ameingia katika tuhuma hizo baada ya kutoa majibu yenye ukakasi bungeni
alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya vilabu kuwa na viwanja vyake na jitihada ya
serikali kuboresha viwanja vya michezo hapa nchini.
Kwa upande
wake Katibu wa chama cha soka mkoa wa Arusha alisema kuwa jiografia ya uwanja
huo ni nzuri ila mapungufu machache yanayoukabili uwanja huo ikiwemo sakafu ya
vyumba vya kubadirishia nguo wachezaji na uhaba wa vyoo vya watazamaji.
“Ni kweli
uwanja huo una mapungufu hayo ila tumeshaongea na meneja wa uwanja kuufanyia
marekebisho uwanja huo kwa mujibu wa maagizo ya TFF yaliyotolewa na raisi wa
TFF Jamal Malinzi mwishoni mwa mwaka jana”
Meneja wa
uwanja huo Andrew Mneja alisema kuwa tiyari mikakati ya kuuboresha uwanja huo
unafanyika ambapo wataufunga wiki ijayo march 25 na tiyari wakandarasi
wameshakagua na wataanza maboresho karibuni ikiwemo kuumwagilia kustawisha
nyasi.
Mwisho………….
0 comments:
Post a Comment