BUNGE limepitisha rasmi Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya
wa mwaka 2014, huku adhabu ya kifo kwa watakaokutwa na dawa hizo,
ikishindikana kuingizwa kwenye muswada huo, isipokuwa mapapa na vigogo
wa biashara hiyo, wameongezewa adhabu ya faini ya Sh bilioni moja na
kifungo cha maisha.
Hata hivyo, baadhi ya wabunge bado wameendelea kung’ang’ania kuwa sheria
hiyo ijumuishe adhabu hiyo kali ya kifo kwa wafanyabiashara, mapapa au
vigogo wanofadhili biashara hiyo, kwa kuwa madhara ya dawa hizo ni
makubwa na yanaathiri zaidi vijana ambao ni nguvukazi ya nchi.
Akitoa majumuisho ya michango ya wabunge kuhusu hoja ya muswada huo,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista
Mhagama, alisema adhabu ya kifo haiwezekani kuingizwa kwenye sheria
hiyo, kwa kuwa adhabu hiyo nchini iko kwenye makosa mawili pekee.
“Ni kweli Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo bado zinatoa adhabu ya
kifo, lakini kwa mujibu wa sera iliyopo, adhabu ya kifo imeingizwa na
kubainishwa kwenye makosa ya uhaini na mauaji pekee,” alisema Mhagama.
Home
»
»Unlabelled
» Bunge la Tanzania laondoa adhabu ya kifo kwa wanaokutwa na dawa za kulevya
Thursday, March 26, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment