.

.
Tuesday, June 4, 2013


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua juu na kunyesha Kitabu cha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua juu na kunyesha Kitabu cha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Asha-rose Migiro, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Makamu, ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, wakiperuzi kitabu cha Katiba mpya, baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo kwenye Viwanja wa Karimjee, jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Tume ya Katiba mpya, baada ya uzinduzi huo.


 Picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali.
 Viongozi wakiwasili
 Meza kuu
 Wananchi na wanasiasa wakifuatilia uzinduzi
Baadhi ya viongozi waandamizi wakifuatilia uzinduzi huo


Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Misri imethibitisha rasmi matokeo ya kura ya maoni na kuipa ushindi kura ya ndiyo na hivyo kupitishwa kwa katiba mpya ya nchi hiyo baada ya asilimia sitini na nne ya wapiga kura kuunga mkono rasimu.

Rais Mohamed Morsi na vyama ambavyo vinamuunga mkono kikiwemo chama tawala cha Muslim Brotherhood ndivyo vimeibuka na ushindi kwenye kura hiyo ya maoni huku upinzani ukindelea kulalama kuwa kumekuwa na hila katika mchakato wa kupitishwa kwa katiba hiyo.
Waziri Mkuu wa Misri Hisham Qandil amesema hakuna upande ambao umeshindwa kwenye kura ya maoni kwa kuwa katiba mpya itakuwa ya wananchi wote kipindi hiki ambacho upinzani unaendelea kupinga.
Kwa upande wake msemaji wa wapinzani wa muungano wa National Salvation Front Khaled Daoud amesema tayari wameshawasilisha madai yao katika ofisi ya Mwendesha Mashtaka kupinga udanganyifu uliofanywa ili kupitisha rasimu ya katiba.
Muungano huo umeapa kuendeleza harakati zake kuhakikisha Wamisri wanapata katiba watakayoichagua wao wenyewe hali ambayo inazua hofu ya kuibuka kwa mzozo zaidi na kuendeleza wimbi machafuko yaliyodumu kwa takribani mwezi mmoja tangu Rais Mursi ajiongezee madaraka.

0 comments:

Post a Comment