.

.
Wednesday, June 19, 2013

7:28 AM

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini godbless Lema pamoja na Mwnykiti wa kambi ya upinzani Bungeni Freman Mbowe wakielekea polisi.

Na Bertha Ismail, Arusha
Jeshi la polisi limewataka Mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kujisalimisha polisi kwa hiari yao wenyewe kama shmu ya kutii shria bila shuruti.

Aidha pia jeshi hilo linawashikilia watu  67 wakiwemo wabunge wanne wa kambi ya upinzani  kwa kosa la kufanya mkusanyiko usikuwa na kibali katika kiwanja cha Soweto jijini hapa.
Akiongea na waandishi wa habari kamishina wa polisi Paul Chagonja Alisema kuwa wanawasaka wabunge hao baada ya kukimbia kusiko julikana mapema jana mara baada ya kufanya mkutano pasipo kuwa na kibali cha mmiliki wa kiwanja(AICC) pamoja na jeshi la polisi .
Aliwataja  wabunge ambao wamekamatwa na jeshi hilo  kuwa ni pamoja na mbunge wa singida Tundu Lissu ,Mbunge viti maalumu Joyce Nkya,mbunge wa Mbulu Mustafa Akunay pamoja na Saidi Arifu ambapo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema kesho mara baada ya kupata mthamana wakiwa katika kituo kikuu cha polisi mkoa
Sanjari na hilo pia kamishina huyo alisema kuwa  jeshi hilo linawataka viongozi hao wawili wa kambi ya upinzani kuja kutoa ushaaidi wa mlipuko wa bomu  uliotokea Jun 15 katika kiwanja cha Soweto wakati mkutano wa chadema wa kufunga kampeni ulipokuwa unafanyika kwani viongozi hao walidai kuwa wanao ushaidi wa kutosha wa picha na video zinazoonyesha muhusika wa kitendo hicho cha ulipuaji wa bom uliosababisha watu 3 kufariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa.
“kama kweli mbowe na lema wanamapenzi mema na wakazi wa Arusha na uchungu wa damu ya wananchi iliyomwagika wajitokeze kulisaidia jeshi la polisi kutoa ushaidi huo ,ili muhusika aweze kufikishwa kwenye vyombo vya dola kwani polisi sio wauaji bali wasimamia ulinzi na haki ya wananchi wake na kama basi wataona hawataki kutoa ushaidi kwetu na wanatuisi vibaya kama wanavyo sema basi wapeleke ushaidi huo kwa Rais wa nchi maana yeye ndie Amiri  jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchi”alisema Chagonja

Aliongeza kuwa kama wataona pia huko apafai kupeleka  basi watafute shehe au padre wapeleke ushaidi huo na hatu kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu huyo ambaye ameusika ,aidha alibainisha kuwa endepo hawata fanya hivyo sheria itafata mkondo wake kama inavyosema kuwa iwapo mtu anaushaidi wa kosa la jinai na anakaa nao pasipo kuutoa   kwa vyombo vya dola basi mtu Yule nae atachukuliwa sheria ya yeye pia kufunguliwa kosa la jinai.

Pia aliwataka wakazi wa mkoa wa Arusha kuendela na shughuli zao huku wakijipusha na makundi ya kisiasa pamoja na mikusanyiko isiyokuwa na kibali  kwani kufanya ivyo ni kuendeleza machafuko huku wahusika wakiwa wanatafuta mkono wao kwenda kinywani .
Aidha aliwataka waandishi wa habari kuwa wazalendo kwa nchi yao na kutumia kalamu  pamoja na kamera zao kulinda na kutunza amani ya nchi ikiwemo  kuheshimimu sheria kwa kuandika habari za kweli zenye kulinda amani kuliko kuleta machafuko.

Aidha watu hao wakiwmo na wabunge wao wameachiwa mapema leo kwa mdhamana hadi hapo juni 21 watakaporudi tena.

0 comments:

Post a Comment