KLABU
ya Galatasaray ya Uturuki imefufua mazungumzo na Chelsea na ipo tayari
kutoa Pauni Milioni 16 kumnunua kiungo Mnigeria, John Obi Mikel.
Mtaalamu
huyo aliungana na The Blues mwaka 2006 - akisajiliwa na Jose Mourinho -
baada ya mzozo mkubwa wa usajili uliozihusisha Manchester United na Lyn
Oslo ya Norway.
Lakini
anaweza kuondoka baada ya miaka sita mara tu baada ya kocha huyo
kurejea Chelsea, na klabu hiyo ya Uturuki ipo tayari kumnasa.
Yuko njiani? John Obi Mikel, aliyeichezea Nigeria katika Kombe la Mabara, anaweza kujiunga na Galatasaray akitokea Chelsea
Kifaa: Kiungo Mikel amekuwa Stamford Bridge tangu ajiunge na timu hiyo mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 19 kutoka Lyn Oslo
Dili
hilo litafanya Mikel aungane tena Didier Drogba, ambaye amejiunga na
Galatasaray msimu uliopita baada ya kuondoka Chelsea kuhamia Shanghai
Shenhua ya China.
Mikel
amebakiza miaka minne katika Mkataba wake Stamford Bridge, lakini akiwa
kwenye Kombe la Mabara na Nigeria alisema mustakabali wake ni tata.
"Nina
miaka minne katika mkataba wangu na Chelsea, lakini unafahamu, katika
soka huwezi kubashiri, siku moja upo hapa, siku inayofuata unaweza
kuondoka,"alisema.
Walipokuwa pamoja: Akihamia Galatasaray, Mikel ataungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba
0 comments:
Post a Comment