Na Bryceson Mathias, Morogoro.
WANDISHI
waandamizi wa Vyombo vya Habari nchini,Wamemshutumu moja kwa moja Spika
wa Bunge, Anne Makinda, wakimtuhumu kuwa kuwa anaongoza kudhalilisha
Utu wa Wandishi na Vyombo wa Habari.
Wakizungumza
katika mahojiano ya Jicho letu ndani ya habari Julai 13, 2013 kujadili
Rasimu ya Katiba, Mhariri wa Gazeti la Jamhuri Deodatus Balile alisema,
“Mimi Simung'unyi Maneno, Spika Makinda anaong
oza kwa kuvidhalilisha Vyombo vya habari na Utu wa Wandishi”.alisema Balile.
oza kwa kuvidhalilisha Vyombo vya habari na Utu wa Wandishi”.alisema Balile.
Upande
wake, Allan Lawa, wa Baraza Habari Tanzania (MCT) alisema, Spika
anafanya hivyo akijua fika kuwa aliwahi kuwa Waziri katika Ofisi ya
Waziri Mkuu akishugulikia Habari’
Walidai,
wanamshangaa Makinda kudhalilisha Wandishi na Vyombo vya habari na
kuwaita Wanahongwa na Wabunge ili wawaandike vizuri, lakini amesahau
kuwa wakati wa Mchakato wa Ubunge wake na kinyang’anyiro cha U-Spika,
vilimsaidia na hakusema vinahongwa!.
Mtangazaji
Dotto Bulendu aliongoza majadiliano Startv-Mwanza na wageni Balile na
Lawa, na Stumai Gerge alikuwa na Mhadhiri wa Shule Kuu ya Uandishi wa
Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam,
Dk. Ayub Rioba na Pili Mtambalike wa MCT,
Rioba
alisema, ziko Demokrasia za aina Mbili ya kuletwa ambayo katika
utekelezaji wake huwa na maslahi kwa walioileta, na ile iliyoibuliwa na
wananchi (created) utekelezaji wake una faida kwa wahusika, na kusema
Rasimu haikuandika na Jaji Joseph Warioba pekee, ila wajumbe wote 30,
akihofu vitu vilipitishwa Warioba akiwa hayupo .
Aidha,
Pili Mtambalike (MCT), akihojiwa na Stumai alisema, kuna maeneo ya
Rasimu katika Uhuru wa Habari lazima yapitiwa upya; ili tusirudi tena
nyuma kwenye Sheria gandamizi kwa wandishi na ugumu wa kupata habari,
“tunakwenda mbele haturudi nyuma”.alisema Mtambalike!
Mbali
ya waandishi kusema ukikiandika Chama tawala mwandishi unaonekana
Mchochezi na kupendelea Upinzani, na ukikiandika Chama pinzani
unaonekana Mzalendo, Wachangiaji nchini pia walipigilia Msumari
wakiwaunga Mkono wandishi wakidai, habari zao kamaa Waajiri zinapuuzwa,
wanasia ambao ni waajiriwa ni kipaumbele kwa watawala.
0 comments:
Post a Comment