.

.
Wednesday, July 3, 2013

Dida akiwa mazoezini na Yanga SC Loyola leo
Na Baraka Kizuguto,

KIPA mpya aliyesajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC, Deogratius Munishi 'Dida' pamoja beki wa kati aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, Rajab Zahir leo wameanza rasmi mazoezi na timu yao Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Deogratius Munishi 'Dida' ameungana na wachezaji wengine wawili mshambuliaji Shaban Kondo aliyekua akicheza soka nchini Msumbiji pamoja na Zahir aliyerejea kutoka nchini Afrika Kusini alipokuwa akifanya majaribio katika timu mbili za Ligi Kuu nchini humo.
Mapema jana katika siku ya kwanza ya mazoezi kiungo mshambuliiaji Mrisho Khalfan Ngassa alifanya mazoezi asubuhi chini ya kocha mholanzi Ernest Brandts kabla ya kocha huyo kuwapa nafasi wachezaji wote wa timu ya taifa, Taifa Stars kujiunga na timu hiyo leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Uganda julai 13 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Rajab Zahir

Hadi sasa klabu ya Yanga imefanikiwa kusajili wachezaji watano wapya ambao ni Dida kutoka Azam, Zahir wa Mtibwa, Ngassa wa Simba, Shaban Kondo aliyekuwa Msumbiji na Realitus Lusajo kutoka Machava FC.
Kocha Brandts amefurahia kuongezeka kwa wachezaji hao kwani amesema atapata fursa ya kukaa nao na kucheza michezo ya kirafiki kanda ya ziwa hali itakayopelekea kupata nafasi ya nzuri kukiandaa kikosi na msimu mpya wa 2013/2014.
Yanga itaendelea na mazoezi kesho asubuhi Loyola ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ziara yake Kanda Ziwa inayotazamiwa kuanza mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.
Wachezaji wote wameendelea na mazoezi leo asubuhi isipokua wachezaji waliojiunga na kambi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda.

0 comments:

Post a Comment