Waziri
Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye amewatahadharisha Watanzania kuwa makini
na watu wanaotaka madaraka kwa kugawa fedha katika sehemu mbalimbali za
nchi au majimbo akionya wanaweza kujikuta wakimweka madarakani kiongozi
anayejihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
“Hivi
kama mtu anaweza kuhonga sehemu kubwa ya wapigakura katika jimbo la
uchaguzi au hata katika nchi kama nafasi anayosaka ni urais;
tumeshajiuliza hizo fedha nyingi hivyo anapata wapi? Kama anajihusisha
na biashara hizo chafu akipata nafasi hiyo watoto wetu watapona?”
alisema Sumaye jana na kuongeza:
“Haya ni
maswali muhimu ya kujiuliza tunapoelekea mwaka kesho kwenye uchaguzi wa
Serikali za Mitaa na mwaka 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu.”
Alisema hayo mjini Morogoro kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata).
Akizungumza
kwa tahadhari alisema haizungumzii Serikali yake iliyoko madarakani
wala mtu yeyote, bali tabia mbaya, Sumaye alisema biashara ya dawa za
kulevya inahusisha fedha nyingi na mitandao mipana ambayo isipodhibitiwa
inaweza kulitumbukiza taifa katika janga.
Alisema
Katiba Mpya siyo mwarobaini wa matatizo yanayolikabili taifa bali,
utekelezaji na usimamizi wa sheria na kwamba jambo muhimu ni kuwa na
Serikali itakayosimamia na kutekeleza sheria ili kulinda yale
yaliyoelekezwa katika Katiba.
“Katiba
haiwezi kumzuia mwizi kwenda kuiba na sheria haitamzuia mwizi kwenda
kuiba ila itatamka adhabu ya kupewa huyo mwizi. Kwa hiyo ili vyote hivi
viwe na maana ni lazima awepo mtu au chombo cha kumkamata huyo mwizi na
kumfikisha katika mikono ya sheria na chombo hicho ni Serikali. Kama
haiwezi kufanya hiyo kazi kwa ukamilifu tutaishia kulalamika tu na
maonevu na maumivu yataendelea kuumiza jamii.”
“Kwa hiyo
hata Katiba iwe nzuri namna gani na ikatamka kuwa rushwa ni adui wa
haki na hata ikatoa adhabu kali sana kwa kosa hilo; kama tutaweka
viongozi madarakani kwa rushwa, hiyo Katiba wala haitatusaidia. Hivyo
Katiba nzuri mpya lazima iambatane na Serikali safi yenye kusimamia
masilahi ya umma. Huwezi kumweka madarakani mwenyekiti wa kijiji au
diwani au mbunge au hata Rais kwa rushwa ya kuwanunua wapigakura halafu
utegemee Katiba Mpya itajibu matatizo ya jamii.”
Azungumzia Mviwata
Sumaye
alisema Mtandao huo wa Wakulima Wadogo Tanzania ndiyo unaojua tatizo la
kilimo na shida zao na ndiyo unaotakiwa kuulizwa cha kufanya ili kilimo
chetu kibadilike na mkulima afaidike...
“Kama
hatuwahusishi na kuwashirikisha katika sera, mipango na programu za
kilimo, basi tujue kuwa sera, mipango na programu hizo zitashindwa.”
Alisema
Tanzania ni nchi ambayo wananchi wake wengi wanategemea kilimo kwa
maisha yao na uchumi wa taifa pia kwa kiasi kikubwa hutegemea sekta
hiyo, lakini bado ni duni na hakijamkomboa mkulima mwenyewe wala uchumi
wa taifa... “Nchi na watu wake bado ni maskini pamoja na kuwa watu
wachapakazi wapo na ardhi kubwa na nzuri yenye rutuba ipo
0 comments:
Post a Comment