.

.
Wednesday, March 18, 2015


MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, leo ameongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa kumuuaga mwili wa marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu ‘Marsh’,yaliyofanyika uwanja wa Shule ya msingi Mirongo Jijini Mwanza.
Meya wa Jiji la Mwanza , Stanslaus Mabula alisema,jiji la Mwanza akielezea wasifu wa marehemu Marsh, ikimbukwe kuwa Mstahiki ndiye mlezi wa kituo cha soka cha Marsh Academy.
Mchezaji wa zamani wa Yanga na Timu ya Taifa Stars, Edibily Jonas Lunyamila (kushoto) akielezea alivyomfahamu marehemu Marsh, na kulia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Pamba, Yanga na Taifa Stars. Fumo Felician akiwa na majonzi.
Msanii wa tasnia ya filamu nchini Steve Nyerere akitoa ushuhuda wake.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu akitoa salamu za rambirambi na kuelezea jinsi Marsh alivyokuwa mwaminifu na kuwa mwanachama hai hata kwenye nyanja za siasa, wengine ni makatibu wa chama hicho toka wilaya mbalimbali mkoani Mwanza.

Familia.
Viongozi na wadau wa soka.

Hassan kiraka akiwa amemshika mkono kumuongoza mmoja ya watoto wa kituo cha Marsh Academy.

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya H.Baba akitoa heshima zake za mwisho.
Safu ya viongozi ni huzuni tupu....
Nini hatma ya vijana hawa wa kituo cha soka cha Marsh Academy.

Huzuni kwa timu ya U17 toka kituo cha Marsh Academy.

Sehemu ya umma uliofika eneo la tukio.
Sehemu ya umati uliwakilisha makaburini.
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, leo ameongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa kumuuaga mwili wa marehemu Sylvester Balunzi Mashishigulu ‘Marsh’,yaliyofanyika kwenye makaburi ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza.

Pia katika mazishi hayo, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, aliwaongoza waombolezaji katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na viongozi wa serikali na  vyama vya siasa, madhehebu ya dini,wananchi, wadau wa michezo,wanasoka wa vizazi mbalimbali ,makocha na waamuzi kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Mulongo aliwaasa waombolezaji waliojitokeza kuaga mwili wa kocha huyo kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mirongo kuwa ,ili kumuenzi kwa vitendo ,wadau wa soka mkoani hapa wachague timu moja na uwanja utakaoitwa jina lake.

Mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza, aliutaka uongozi wa chama cha Soka mkoa wa Mwanza (MZFA) waandae programu ya kuanzisha michuano ya mpira wa miguu itakayofanyika kila mwaka na kuiwasilisha ofisini kwake ikiwa na lengo la kumuenzi kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji vya vijana na kuviendeleza kama ilivyokuwa dhamira ya marehemu.

Aidha Mgeja akimzungumzia marehemu alisema marehemu Marsh aliwea kujitolea kuitangaza Mikoa Mara, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Dar es salaam na  taifa katika medani ya kimataifa,wakati akifundisha vilabu mbalimbali vya hapa nchini ikiwemo timu za taifa ya vijana Serengeti boys na Taifa stars.

Kwa wake Meya wa Jiji la Mwanza , Stanslaus Mabula alisema,jiji la Mwanza litatenga viwanja vya michezo kwa ajili ya kuibua vipaji vya vijana wadogo wa lika tofauti zaidi ya 200 kwa nyakati tofauti na  ambao marehemu alikuwa akiwahangaikia  kuwalea kwa maisha ya soka katika maisha ya uhai wake.

“Amekuwa mwanzilishi wa vitalu vya kuendeleza mchezo wa soka mkoani na nchini hapa,matunda yake yameonekana kwa kutoa vijana wenye uwezo ambao wameweza kutoka nje kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa lakini pia wapo wanaocheza katika vilabu vya  Ligi Kuu nchini,”alisema Mabula.

Wadau mbalimbali wa soka wakiwemo wachezaji wa zamani na wa kizazi cha sasa, walionesha masikitiko yao makubwa kwa kumpoteza mtu muhimu katika familia ya soka,kwamba pengo lake haliwezi kuzibika kutokana na mchango wake wa kuendeleza mpira wa miguu nchini katika maeneo aliyofanyia kazi ya ukocha.

Diwani wa Kata ya Mirongo Daudi Mkama (CUF) alimpongeza Meya wa Jiji la Mwanza Mabula kwa moyo wake wa kujitolea na kuamua kugharamia sehemu kubwa ya mazishi ya marehemu Marsh tangu kuwasili kwake, kuagwa na kupelekwa nyumbani kwao Igoma na wananchi wa maeneo hayo kutoa heshima za mwisho kabla ya kushiriki mazishi yake yaliyofanyika makaburi ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza.

"Munyonge munyongeni na mtu anayefanya jambo jema hatuna budi kumsifia na kumpongeza, kwa hili alilolifanya Mstahiki meya wa Jiji, Mabula la kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa kwa asilimia 90 ni kuonyesha ameguswa lakini kama kiongozi wa watu ametekeleza wajibu wake kwa moyo wake wa kujitolea,"alisisitiza Mkama.

Wadau wa soka kutoka mikoa mbalimbali nchini wakiongozwa na RC Mulongo, Meya Mabula, DC Baraka Konisaga (Nyamagana), DC Angelina Mabula (Iringa), Kocha na Mwakirishi wa TFF Salum Madadi, Mwenyekiti wa MZFA Jackison Songola, Mbunge wa Jimbo la Rorya - Mara Lameck Airo (CCM) kumuaga na kisha mazishi yake kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja, wananchi na wadau wengine.

0 comments:

Post a Comment