.

.
Monday, March 23, 2015

4:17 AM
na Bertha Ismail - Arusha

Bingwa wa kimataifa wa mbio za baiskeli mtanzania Richard Laizer ameng,ara katika mbio za taifa na kuibuka mshindi wa kwanza baada ya  kuwazidi washindani wenzake zaidi ya 70 kutoka mikoa sita ya Tanzania bara.

Laizer kutoka Arusha aliyerejea hivi karibuni kutoka Afrika ya kusini alitumia muda wa saa 3:27:01 kunyonga baiskeli yake umbali wa kilomita 133 na kujishindia kitita cha shilingi laki nne, akifuatiwa na anaeshikilia ubingwa wa taifa Hamis Hussein aliyemaliza wa pili kwa kutumia saa 3:28:30 na kujishindia shilingi laki mbili huku mpanda baiskeli kutoka mwanza Sunga Duba alikiibuka wa tatu kwa kutumia saa 3:28:40 kumaliza mbio na kujishindia laki moja na nusu taslim.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na club ya Arusha cycling kwa lengo kujifua kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya kimataifa yalishirikisha washindani wa kitaifa na kimataifa ambapo vijana ( 20- 45) walichuana kumaliza mapema kilometa 133 huku wanawake na vijana wadogo (under 20) wakichuana kwa kilometa 80 pamoja na  wazee (45-..)ambao wengi wao walitoka mataifa ya ulaya , Amerika na Australia.

Kwa upande wa wanawake mpanda baiskeli mkongwe Sophia Hussein aliibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia saa 3:10:05 na  kufuatiwa na mpinzani wake Sofia Adson aliyetumia saa 3:22:11 huku mpanda baiskeli chipukizi Jamila Jumanne akimaliza wa tatu kwa kutumia saa 3:55:14 wote wakiwakilisha mkoa wa Arusha.

Wageni toka nje ya nchi walitamba katika mbio za wazee baada ya Steven Charmly toka Australia kushika nafasi ya kwanza na kufuatiwa na Thaday Peterson toka Amerika aliyekuwa pili na wa tatu akiwa ni Hendry Banderland kutoka Uholanzi.

Kadhalika kwa upande wa vijana wadogo, Kijana chipukizi Kelvin Didas (14) aling’ara katika mbio hizo na kuwakilisha vema baada ya kuwatoka wenzake umbali mrefu na kufuatiwa na David Philemon huku nafasi ya tatu akiibuka Mussa Husein wote kutoka mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari baada yam bio hizo, katibu msaidizi wa Arusha Cyclin Club, Thaday Peterson alisema kuwa mbali na kuvutiwa na mabadiliko makubwa ya msichana Sophia Hussein aliyeshika namba moja kutokana na kumshirikisha mashindano ya kimaifa Afrika Kusini msimu uliopita lakini zaidi amevutiwa na vijana wadogo.

“Kiukweli Sophia baada ya kushiriki mashindano ya Afrika kusini ameonyesha mabadiliko makubwa, lakini ukiachana na hayo uwezo walionao hawa vijana wadogo pia ni mkubwa sana hali inayovutia kuwekeza zaidi kwao hasa katika kuwashirikisha katika mashindano ya kimaifa na hii imetufanya sisi tuwe na kiu ya kuwatafuta vijana wadogo zaidi kwa wanaume na wanawake ili kutusaidia kufanya vema zaidi”


Mwisho…………………………..

0 comments:

Post a Comment