.

.
Wednesday, March 18, 2015

12:48 AM
na Bertha Ismail - Arusha

Viongozi wa zamani wa chama cha soka wilayani Arusha ADFA wanajipanga upya kuingia madarakani katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika wakati wowote kuanzia sasa kufuatia uongozi uliopo madarakani kumaliza muda wake.

Viongozi hao wakiongozwa na katibu wa zamani wa ADFA Robert Munis wamekuwa wakifanya vikao vya kupanga mikakati madhubuti wa kuwang,oa madarakani kamati yote ya utendaji ya ADFA kwa kigezo cha kuporomosha soka la Arusha kwa kuvipa vilabu mzigo wa michango mbali mbali ikiwemo ada kubwa ya ushiriki ligi hali ambayo timu nyingi zenye uwezo zimekwama kushiriki ligi za taifa kuanzia ngazi ya wilaya hadi mkoa.

Hadi sasa vikao zaidi ya vinne vimeshafanyika katika mgahawa maafuru unaojulikana kama Spice Inn uliopo pembezoni mwa uwanja wa Sheih Amri Abeid na kushirikisha wajumbe wa zamani wa ADFA akiwemo Hessein Lembarity aliyekuwa mwenyekiti, Abdul kondo aliyekuwa mjumbe na mkurugenzi wa rollingstone Ally Mtumwa aliyewahi kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF.

Akizungumzia lengo lao hilo la kurudi kwenye uongozi, Robert Munis anasema yeye alistaafu kwa hiyari yake baada ya kuwa katibu kwa zaidi ya miaka 10 kutokana na kuzidiwa na maswala na kazi na familia huku akiamini atakaowaachia wataendeleza mema yale ikiwemo kuziongeza timu nyingi kushiriki ligi mbali mbali sambamba na kubuni mashindano mengine mengi kuongeza idadi ya yaliyokuwepo lakini hali haikuwa hivyo.

“Unajua mimi nilizidiwa na maswala yangu ya kazi na familia hivyo nikabidi niachie ngazi moja nishikilie familia na kazi yangu huku nikiamini hawa nitakaowaacha watafanya muendelezo lakini nasikitika sana kusikia eti soka la Arusha sasa limedorora na mashindano mengi yaliyokuwepo yamekufa hali ambayo ni mbaya sana timu kufanya mazoezi pekee kwa ajili ya ligi ya Taifa”

“Hivyo basi kama mdau wa soka mkoa huu sitakubali kuona soka la Arusha linakufa kifo cha aibu kiasi hiki kutokana na uzembe ulioko madarakani ni bora tuwaondoe turudi tufanye kazi na niombe wadau wa Arusha wajitokeze kuunga mkono hili lifanikiwe kurudisha heshima ya Arusha kuwakilishwa na timu mbili hadi taty ligi za juu (daraja la kwanza na ligi kuu)” alisema Robert alieonekana wazi kujaa jazba.

 Alisema kuwa sasa analazimika kurejea kwa kishindo baada ya kusikitishwa na kuporomika kwa soka la Arusha na kutengwa kwa soka la Arusha na wadau mbalimbali wakiwemo wafadhili, wafanyabiasha na viongozi wa kitaifa ambapo alisema kuwa chanzo cha kudorora kwa soka.


Inasikitisha mkoa wa Arusha uliowahi kuwa na timu tatu ligi kuu sasa hakuna hata timu moja na hata michezo ya kimataifa iliyokuwa ikichezwa Arusha sasa haichezwi achilia mbali kuharibika kwa uwanja wa sheikh Amri Abeid kutokana na kujaa mashimo kila upande huku vichuguu vikichipuka kila pembe na majani yake kunyauka kutokana na viongozi wa soka kufumbia macho swala hili, huku viwanja vingine tegemezi vikifungwa bila uongozi kuomba upendelea kwa timu kufanyia ,mazoezi na mashindano.

Aidha uchaguzi wa soka ngazi za wilaya za mkoa wa Arusha zinatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia mwezi Aprili huku wagombea wa nafasi mbali mbali wakipigana vijembe chini chini kuwania nafasi hizo lakini wengi wao wakitupia lawama uongozi wa sasa na kuwa na nia moja ya kuwang’oa madarakani.

Mwisho……………………..

0 comments:

Post a Comment