.

.
Thursday, March 26, 2015

kamanda Liberatus Sabas


na Bertha Ismail - Arusha

Jeshi la polisi mkoani Arusha limewataka wakazi wa Arusha kujitokeza kuutambua mwili wa mwanamke mmoja mwenye umri kati ya miaka 18-20 aliyekutwa amefariki huko eneo la mjini kati jirani na ofisi ya CCM mkoa.

Akizungumza na gazeti hili, kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, kamanda Liberatus Sabas alisema kuwa mwili huo uliohifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya mkoa, Mount Meru umeokotwa mapema jumatatu march 23 mwaka huu ndani ya Carvati liliopo eneo la CCM mkoa.

Alisema mwili wa mwanamke huyo bado haujatambuliwa  hadi sasa jina wala makazi yake ambapo inasadikika marehem alifariki na kukaa hapo zaidi ya wiki moja huku chanzo cha kifo kikiwa hakijafahamika hadi sasa ambapo mwili huo umegundulika kutokana na harufu kali iliyokuwa inatoka kwenye eneo hilo.

“Baada ya watu kusikia harufu hiyo ndio kuchunguzwa inapotokea na kubainika kuwepo kwa mwili huo ulioanza kuoza na jeshi la polisi kwa kushirikiana na zima moto walifanikiwa kuutoa na kuuhifadhi mount meru.

Wakati huo huo jeshi la polisi limefanikiwa kukamata magunia 11 ya madawa ya kulevya aina ya bhangi na mtu mmoja aliyekuwa akisafirisha huko maeneo ya bara bara ya Arusha / Namanga wilayani Longido mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi, Kamanda Sabas alisema kuwa madawa hayo yalikuwa yakisafirishwa kutoka Arusha kuelekea Longido kupitia gari Toyota land Crusa Pick-up yenye namba T.695 ARR Mali ya kampuni ya uwindaji ya Wengert Windrose iliyokuwa ikiendeshwa na Frank Faustine (40).

“Kufuatia tukio hilo, pia tunamshikilia dereva huyo Frank Faustine kwa upelelezi zaidi na akibainika kuhusika sheria itachukua mkondo wake, ila naomba kutoa wito kwa wakazi wa Arusha kuacha kujishughulisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na wafanye biashara halali ya kujipatia kipato” alisema Sabas

Mwisho……………….

0 comments:

Post a Comment