.

.
Wednesday, April 9, 2014

10:35 PM
CHAMA cha Ushirika cha Wakulima wa Korosho Tandahimba – Newala (Tanecu) kinatarajia kuzindua maghala ya kuhifadhia korosho katikati ya mwezi huu ikiwa ni hatua za awali za ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga baada ya ziara ya kutembelea kiwanda cha kusindika maziwa cha Tanga Fresh, Mwenyekiti wa chama hicho, Yusuph Nannila, alisema Rais Jakaya Kikwete ndiye atakayefungua maghala hayo.
Alisema hatua iliyofikiwa mpaka sasa ni kukamilika kwa hatua za mwishoni za maghala hayo ambapo kwa upande wa ujenzi wa kiwanda, wameshapokea michoro  na kwamba kiwanda wanatarajia kujengwa kwa ubia kati ya chama chake na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB).
Nannila alikipongeza Kiwanda cha Tanga Fresh kwa kumudu ushindani wa soko la ndani wakati korosho zinategemea zaidi soko la nje ambalo halina uhakika na halimnufaishi mkulima.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa, Rajabu Kihara, alisema siri ya mafanikio waliyopata katika chama hicho mpaka kuanzisha kiwanda ni ushirikiano mzuri na wanachama wao pamoja na uaminifu wa viongozi wao.

0 comments:

Post a Comment