.

.
Wednesday, April 30, 2014na Bertha mollel -Arusha
 
Kamati ya Olympic Tanzania (TOC) imeahidi kuwapa Shirikisho la mchezo wa tae kwon do Tanzania TTF wataalmu na wakufunzi  wa mchezo huo toka korea na japani ukiwa ni mkakati wa kukuza na kuendeleza mchezo huo wa kupigana karate ya kutukia mikono na mateke.

Rais wa TTF Ally Ramudh akizungumza na Tanzania Daima  mkoani hapa alisema kuwa kamati hiyo ya TOC imeona jinsi Tanzania tulivyo na juhudi za mchezo huo ingawa hatujui utaalam wake sana hali iliyowavutia na  kuahidi kuleta wataalam watakaotuwezesha kujua zaidi.

Alisema mpango huo unaodhaminiwa na kamati ya Olypic ya kimataifa (IOC) umetokana na mafanikio ya kukubalika kwa mchezo huo ambao kwa mara ya kwanza utatoa wawakilishi wa Tanzania katika mashindano yajayo ya Olympic.

Kwa mujibu wa Ramudh wataalam hao wanatarajiwa kutua nchini mwanzoni mwa mwezi wa sita, watazunguka Tanzania nzima kufundisha na kuhamasisha mchezo wa tae kwon do ambapo asili yake ni nchini korea na hong kong.

Akizungumzia juu ya mchezo huo Rais huyo wa TTF alisema kwa sasa mchezo huo umekubalika na kukua kwa kasi kwani sasa unafundishwa katika taasisi mbalimbali za kiusalama kama makampuni ya ulizi na hata katika majehi ya ulinzi na usalama ikiwemo katika majeshi yetu ya polisi.

Tae kwo ndo ni mcheza wa kujilinda kwa kushambulia kwa kutumia mikono na miguu na umejijengea umaarufu mkubwa kwa kuwawezesha mchezaji wa mchezo huu kujilinda hata akishambuliwa na kundi la watu wenye silaha.

Mchezo huo wa Tae kwo ndo ni jamii ya michezo ya  karate ,kong fu na kick boxing wenye asili ya china,korea na japan ambapo humwezesha mtu pia kuwa m’bunifu katika kujihami ambao pia huleta burudani katika kuucheza na kuungalia watu wakiucheza.

0 comments:

Post a Comment