.

.
Friday, April 11, 2014

mbunge wa jimbo la Simanjiro Christopha Ole Sendeka akivishwa skafu mara baada ya kuwasili katika mji mdogo wa Mererani kuzindua mbio za pikipiki zilizoandaliwa na umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) kwa ajili ya kuuenzi muungano wa serikali mbili
mbunge wa jimbo la Simanjiro Christopha Ole Sendeka  alipowasili katika mji mdogo wa Mererani uliopo Simanjiro kuzindua mbio za pikipiki zilizoandaliwa na umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) kwa ajili ya kuuenzi muungano wa serikali mbili, akifungua tawi la wakereketwa
maandamano ya pikipiki yalipokuwa yakimpokea mbunge wa Sinanjiro Olesendeka alipokuja kuzindua mbio hizo zilizoandaliwa na UVCCM kwa ajili ya kuunzi muungano
Mbunge wa jimbo Simanjiro Christopha Ole Sendeka aliwataka watanzania kutumia fursa ya mchakato wa mabadiliko ya katiba kujipatia katiba bora itakayoongoza nchi na siyo kutumia fursa hiyo kama sehemu ya kuuvunja muungano wa jamhuri ya muungano wa TAnzania.

Sendeka aliyasema hayo mwishoni mwa wiki hii alipokuwa akizindua mbio za pikipiki katika mji mdogo wa Mererani iliyopo wilayani Simanjiro mkoani Manyara zilizoandaliwa na UVCCM kwa lengo la kuuenzi muungano wa serikali mbili ambapo walikuwa na kauli mbiu isemayo "Mbili yatosha Tatu ya nini"?


0 comments:

Post a Comment