.

.
Wednesday, April 9, 2014

JK achaguliwa kuwa Rais Bora AfrikaWAKATI kamati 12 za Bunge Maalumu  la Katiba leo zikitarajiwa kuanza kuwasilisha ripoti za majadiliano waliyokuwa wakiyafanya katika sura ya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba, mijadala yao ilitawaliwa na lugha za maudhi, kuonyeshana ubabe na kudhalilishana.
Hata hivyo maamuzi ya kamati nyingi yalishindwa kufikiwa kutokana na kukosa uungwaji mkono wa theluthi mbili ya wajumbe kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar kama kanuni ya 36 (4) ya Bunge Maalumu linavyotaka, ambapo ili ibara ipate kuridhiwa lazima idadi hiyo ya wajumbe ifikiwe.
baadhi ya kamati wajumbe walifikia hatua ya kutuhumiana kwa mambo binafsi ikiwemo kutokuwa na familia au kuwa na mahusiano ya jinsia moja.
Hatua hiyo ilitokana na baadhi ya wajumbe kutoka Zanzibar kutofautiana juu ya muundo wa serikali ambapo wengine walikuwa wakitaka tatu huku wenzao wakitaka serikali mbili.
Tofauti hizo zilisababisha wajumbe wengine kutoleana kashfa za uhusiano binafsi ikiwemo kutokuwa na watoto au mke (ushoga).
Tuhuma hizo ziliwafanya wajumbe wa kamati moja kutaka kushikana mashati, jambo lililoibua taharuki kubwa miongoni mwa wajumbe.
Kamati hizo pia zilitawaliwa na mizengwe ya kutoaminiana ikiwemo ile ya kupinga taarifa za walio wachache ndani ya kamati kuhaririwa na walio wengi.
Kwa mujibu wa kanuni ya 33, Bunge litakuwa na fursa ya kupata ripoti kutoka katika kila kamati ambapo itabeba maoni ya walio wengi pamoja na ya wachache walioshindwa kukubaliana na kile kilichokubaliwa na wengi.
Maoni ya wengi na ya wachache huunganishwa katika ripoti moja inayosomwa na mwenyekiti wa kamati huku mmoja wa wale wajumbe wachache akisoma yao kisha Bunge kuyajadili.
Baadhi ya wajumbe walilalamika kwamba kulikuwa na mipango ya wenyeviti wa kamati hizo kutaka kuhariri maoni ya wachache ambayo inadaiwa yamekuwa na maneno makali ya kuishambulia serikali na chama tawala (CCM).
Mipango hiyo iliwafanya wajumbe wachache kupinga kuhaririwa kwa taarifa zao huku wakitoa hoja kuwa hawakushiriki kuandaa taarifa za wengi hivyo nao hawapaswi kuingiliwa kwenye uandaaji wa taarifa zao.
mipango ya kuhariri taarifa za walio wachache hata hivyo hazikufua dafu kwakuwa baadhi ya wajumbe walishikilia msimamo wao na kutoa taarifa kwa uongozi wa Bunge kuhusu hila hizo. Inadaiwa kuwa baada ya uongozi wa Bunge kudokezwa jambo hilo ulilitolea ufafanuzi kuwa taarifa za walio wachache zisihaririwe na viongozi wa kamati bali ziachwe kama zilivyoandaliwa na wahusika.
Wenyeviti wakabidhi ripoti
Jana wenyeviti wa kamati mbalimbali walikuwa wakikabidhi ripoti za kamati zao kwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge, Samia Suluhu Hassan, tayari kwa kuingizwa kwenye orodha za shughuli za Bunge Maalumu.
Mwenyekiti wa Kamati namba tano, Hamad Rashid Mohamed, alisema kuwa kamati yake ilichambua mambo mbalimbali kadiri walivyokuwa wamepata maelekezo ikiwa ni pamoja na kuandika mapendekezo ya walio wengi na wachache.
“Kwa leo mimi mimewasilisha ripoti nzima lakini wakati wa kuwasilisha katika Bunge Maalumu mimi nitawasilisha ripoti ya walio wengi na walio wachache watawasilisha wao na hata ripoti wameiandika wao,” alisema Mohamed.
Naye Mwenyekiti wa kamati namba tisa, Kidawa Khamisi Salehe, alisema kamati yake ni kati ya kamati ambazo katika kupiga kura ya siri na wazi ilifanikiwa kutimiza theluthi mbili kila upande.
“Kamati yetu imefanikiwa kukamilisha theluthi mbili kila kipengele na tumefanya vikao vyetu kwa amani na tumejadili kwa kina na hatimaye tumefikia hapa tulipo.
“Tumewasilisha ripoti yetu katika Ofisi ya Bunge ili ipitiwe na kuzalishwa nakala nyingi ili iweze kugawiwa kwa wajumbe na ijadiliwe bungeni,” alisema Kidawa.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge, Samia Suluhu Hassan, alisema ofisi yake inafanya kazi ya kupokea ripoti kutoka kwa kamati mbalimbali.
Hata hivyo alisema ofisi yake imejipanga kuhakikisha inazalisha nakala nyingi ili zigawiwe kwa wajumbe kwa lengo la kutoa fursa ya kuzipitia mapema na kuanza kujadili.
chanzo: tanzania daima

0 comments:

Post a Comment