.

.
Friday, April 11, 2014Athari za mvua zinavyolikumba jiji la Dar es salaam.
Dar es Salaam. 
Wapo wanaoombea msimu wa mvua uanze ili hali ya joto la Dar es Salaam ipungue, lakini kwa wakazi wengi huwa na maombi tofauti na wakati mwingine wingu jeusi linapotanda tu, taratibu za kuhama makazi yao huanza.
Ni maisha ya mguu ndani mguu nje. Katika maeneo mengi ukipita utaona magodoro na samani nyingine zimeanikwa nje au kuhifadhiwa juu ya paa.


Wanaoishi maeneo ya mabondeni huogopa kulala ndani wakihofu huenda wakasombwa na maji wakati wowote kwa kuwa hata kama mvua hazinyeshi kwenye maeneo yao, bado hufuatwa na maji kutoka maeneo mengine ambako mvua hunyesha.


Katika miaka ya karibuni mvua kidogo tu imekuwa ikisababisha kadhia mbalimbali kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, ikiwemo mafuriko na ongezeko la msongamano wa magari barabarani.


Ongezeko la watu, kuziba kwa mifereji ya kupitisha maji na kujenga katika njia za maji ni baadhi ya sababu zinazotajwa kuchangia kuwafanya wakazi wa Dar es Salaam hasa waishio mabondeni, kukosa usingizi katika kipindi hiki.


Gazeti hili lilifika katika baadhi ya maeneo na kushuhudia familia zikiwa nje ya nyumba zao. Wengine wakiwa wamefungia vitu vyao ndani na kuelekea maeneo mengine wakisubiri maji yakauke ili warudi kuendelea na maisha mabondeni.


Maisha kipindi cha mvua


“Hivi sasa tunaishi kwa machale. Tukiona wingu au mvua imeanza kunyesha tunaondoka. Mali inaweza kutafutwa lakini sio uhai wa mtu,” anasema Madande Jabir mkazi wa Gongo la Mboto.


Jabir anasema mvua ya saa mbili iliyonyesha juzi katika maeneo hayo imesababisha maafa makubwa, ikiwemo kubomoa kuta za nyuma, kuharibu samani na mazao yaliyokuwa shambani.


“Kama isingekuwa machale, ina maana ile nyumba ilipobomoka ingeua watu, lakini tunaishi kwa kujihami na kujibanza popote salama unapoona mvua haiwezi kukubeba,” anasema Jabir.


Wakazi wa Nyaishozi nao wanastaili nyingine ya maisha ambao inasababishwa na maji kujaa ndani ya nyumba zao.


Mwanahamisi Juma anasema maji yameingia mpaka ndani, lakini kwa kuwa si mengi sana, wanalazimika kuendelea na maisha ingawa hali hiyo ina hatarisha

0 comments:

Post a Comment