Chama cha Demokrasia na Maendelo,mkoa wa Arusha(CHADEMA)
kupitia Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Goodbless Lema amemtaka Kamanda wa
polisi Wilaya ya Arusha Mjini ,Bw Gilles Muroto kuomba radhi wananchi hususani
Vijana ndani ya siku tatu mara baada ya Kamanda huyo kusema na kudai kuwa
vijana wa Arusha Mjini ni wavuta bangi
Akiongea na vyombo vya habari mapema leo Mbunge Lema alisema
kuwa kauli ziliztolewa na Kamanda huyo siku ya jana wakati akizuia maaandamano
ya leo ambayo yalikuwa yamepengwa kufanywa na chama hicho
Aidha Lema alisema kuwa wakati kamanda huyo anapita huku
akiwa na gari la Polisi lenye namba za usajili T 1848 aliwatangazia vijana kuwa
wao ni wavuta bangi, na wanywa viroba na mtu yoyote atakayejitokeza kwenye
maandamano basi atavunjwa mguu
Lema aliendelea kudai kuwa kwa kamanda kama yeye hapaswi
kutoa kauli hizo ambazo zinalenga kuchochea uchochezi na ubaguzi ndani ya Mji
wa Arusha badala yake alipaswa kutumia zaidi busara ambayo ingewafanya vijana
hata kama kuna maandamano wasiweze kuandamana
Alifafanua kuwa kwa kuwa ametoa lugha za uchochezi dhidi ya
Vijana ambao wapo ndani ya jimbo lake basi anatakiwa kutumia hilohilo gari la polisi kuomba
radhi wananchi wa jimbo lake ndani ya siku tatu lakini kama hataweza kufanya hivyo
basi wao kama chama wataweza kuchukua hatua
kali zaidi
“jana majira ya mchana katika eneo la Mbauda hadi kwa
Muorombo Kamanda huyo alitoa lugha hizo za Uchochezi dhidi ya Vijana na kudai
kuwa kama Vijana watajitikeza katika maandamano atawavunja miguu sasa huu ni
uonevu tena wa hali ya juu sana hivyo tumeazimia kwa kauli moja kuwa anapaswa
kuomba radhi kwa kauli ambazo amezitoa kama hatafanya hivyo tutaenda mbele
zaidi kwa kumchukulia hatua ili iwe fundisho kwa viongozi wengine”aliongeza
Lema.
Mbali na hayo Lema alidai kuwa suala hilo la kuwatolea
Vijana wa Arusha Mjini maneno kama hayo
ni suala la kukandamiza chama hicho lakini pia katika Kumbukumbu zao
zinaonesha kuwa alishwai kukataa baadhi ya barua ambazo ziliplekwa na Chadema
hali ambayo inaonesha wazi kuwa huo ni ukandamizaji tena wa hali ya juu sana.
“Unapokuwa kiongozi kama OCD unatakiwa kutenda haki kwa
vyama vyote hata kama hukipendi lakini ndio ilishatokea lakini kama unabagua
hadharani hadharani na kutumia kofia yako basi utakuwa ni miongoni mwa watu
wenye dhambi nyingi sana
hivyo basi ni vema kila kiongozi akatenda haki”aliongeza Lema
Hataivyo akiongea kwa njia ya Simu na gazeti hili ili kujibu
shutuma zinazomkabili OCD huyo alidai kuwa yeye sio msemaji wa Jeshi la Polisi
mkoa wa Arusha lakini msemaji ni Kamanda wa Polisi mkoa,wakati naye Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas alidai kuwa mpaka sasa bado hajapokea
malalamiko hayo,hivyo atayafanyia kazi
0 comments:
Post a Comment