Benson Mollel
Aliyekuwa mjumbe wa baraza kuu
la Uvccm mkoani Arusha,Benson Mollel aliyevalia shati la kung’aa
tofauti na wenzake akitoa msaada kwa mtoto aitwaye frank wakati jumuiya
hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa katika hospitali ya mkoa
ya Mt meru hivi karibuni enzi ya uhai wake,anayefuatia ni mwneyekiti wa
uvccm mkoani hapa,Robinson Meitenyiku
MJUMBE wa baraza
kuu la umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi(Uvccm),ngazi ya taifa
kupitia mkoa wa Arusha ,Benson Mollel(26) amekutwa amefariki dunia
ndani ya hoteli ya Lush Garden Bussinnes Hotel iliyopo barabara ya
vijana mkabala na Jacaranda mtaa wa Haile Selassie katikati ya jiji
la Arusha.
Tukio hilo
lililogusa hisia za wengi lilitokea ghafla leo 3 /3/2013 majira ya
saa 6:oo mchana tayari limezua hali ya hofu na mashaka kwa wakazi wa
jiji la Arusha na viunga vyake ambapo tayari limehusishwa na hisia
mbalimbali ikiwemo kulishwa sumu kali.
Kabla ya kukutwa na
umauti alikuwa ni mwanasiasa mchanga ambaye pia alikuwa ni
mfanyabiashara wa madini mkoani hapa ambapo kifo chake kimehusishwa na
masuala ya kisiasa na kibiashara
Marehemu
Mollel,aliutwaa ujumbe wa baraza kuu la Uvccm mkoani Arusha mwaka huu
huku akimrithi mkuu wa wilaya ya Korogwe kwa sasa,Mrisho Gambo katika
uchaguzi uliokuwa na mshike mshike huku akitajwa kuwa kambi ya waziri
mkuu mstaafualiyejiuzulu,Edward Lowasa.
Kwa mujibu wa
vyanzo vya habari ndani ya hoteli hiyo vimedai ya kwamba marehemu
aliwasili mnamo machi 2 mwaka huu majira ya usiku hotelini hapo
akiongozana na mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Nancy ambapo
walichukua chumba nambari 214.
Mmmoja wa walinzi
hotelini hapo aliyejimbulika kwa jina la Obeid Mollel kutoka kampuni ya
ulinzi ya Victoria Support Services ambayo inaimarisha ulinzi hotelini
hapo alisema kuwa marehemu aliingia na mwanamke huyo na kisha kuondoka
ghafla kabla ya kurejea tena wakiwa wote usiku.
Hatahivyo,alisema
kuwa wakati wakiwa hotelini hapo marehemu aliomba kuegesha gari lake
jipya ambalo bado halijapata usajili lenye nambari 4093 gx 110 aina ya
mark ii grande ambapo alikubaliwa na kisha kurejea chumbani na mwanamke
huyo ambaye anatajwa kuondoka leo asubuhi 3/3/2013
Hatahivyo,majira ya
asubuhi mmoja wa wahudumu hotelini hapo(jina lake limehifadhiwa)
alisema kuwa mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maryam
aliwasili hotelini hapo majira ya saa 5;00 na kuomba kupelekwa moja kwa
moja chumba alichokuwepo marehemu.
Mhudumu huyo kwa
sauti ya upole alisema kuwa wakati mwanamke huyo akiomba kupelekwa
chumbani hapo marehemu naye alipiga simu mapokezi na kuomba mwanamke
huyo apelekwe chumbani kwake ambapo walitekeleza jukumu hilo.
Akiendelea
kusimulia tukio hilo mhudumu huyo alisema kuwa walimwona mwanamke huyo
akitoka ghafla nje ya hoteli hiyo majira ya saa 6;00 mchana bila
kumtambua sura yake ambapo hawakufuatilia chochote kwa kujua kwamba
hakuwa na nia mbaya.
“Sisi baada ya
kumwelekeza Yule dada chumba alichofia marehemu hatukufuatilia hadi
pale mlinzi alipomwona akitoka tena nje ya geti wala hakukaa muda
mrefu”alisema mhudumu huyo
Hatahivyo,wakati
hayo yakiendelea mhudumu huyo aliamua kupiga simu ya chumba alichofia
marehemu ili kujua endapo ataendelea kukodisha chumba hicho ama la
lakini katika hali isiyo ya kwaida simu ya chumba hicho ilikuwa
haipokelewi.
Wakati hayo
yakiendelea alisimulia kwamba mmoja wa wahudumu ambaye alikuwa
akifahamiana na marehemu kwa muda mrefu aliamua kumpigia kupitia simu
yake ya mkononi lakini nayo haikupokelewa vilevile.
Baada ya hatua hiyo
mhudumu huyo aliamua kupanda ngazi kwenda chumbani kwa marehemu lakini
katika hali isiyo ya kawaida alikuta mlango ukiwa wazi na mara
alipomwamsha marehemu hakuweza kuamka na ndipo alipotoa taarifa kwa
uongozi wa hoteli na kisha kuviarifu vyombo vya usalama.
Hatahivyo,mhudumu
huyo alipohiojiwa na jamiiblog.co.tz alisema kwamba anahisi nini chanzo
cha kifo cha marehemu huyo alisema kuwa huenda mwanamke aliyekuwa naye
(Maryam) huenda alitekeleza mauaji hayo kwa ustadi mkubwa bila wao
kufahamu.
“Unajua vyumba
vyote vya huko juu ghorofani ukifunga mlango tu huku chini sisi
mapokezi tunasikia sasa cha ajabu mlango tumeukuta wazi na nahisi
alitekeleza haya mauaji akaona asifunge mlango kwa kuwa
tutasikia”alisema mhudumu huyo kwa upole
Jeshi la polisi
liliwasili hotelini hapo majira ya saa 8;00 mchana na kuupakia mwili
wa marehemu kupitia gari lenye nambari za usajili 1477 na kisha
kuufikisha katika chumba cha kuhifadhia maiti ndani ya hospitali ya
mkoa ya Mt,Meru
Akizungumza katika
eneo la tukio mkuu wa jeshi la polisi wilayani Arusha,OCD Gilles Muruta
alisema kwamba jeshi la polisi bado linachunguza undani wa tukio hilo
kwa kuwa limejitokeza ghafla na hapo baadaye litatoa taarifa mwa vyombo
vya habari.
Hatahivyo,katibu
mwenezi wa CCM mkoani Arusha,Isaack Kadogoo alisema kuwa wao wamepokea
tukio hilo kwa mshtuko mkubwa kwa kuwa bado wamepigwa na mashangao kwa
jinsi namna lilivyotokea.
Baadhi ya wanasiasa
wa vyama mbalimbali vya siasa pamoja na wafanyabiashara wa madini
mkoani Arusha waliwasili eneo la tukio nje ya hoteli hiyo ambapo
wengine walishindwa kujizuia na kujikuta wakiangua kilio nje ya hoteli
hiyo.
Baadhi yao,James
ole Milya kada wa Chadema pamoja na Mathias Manga diwani wa CCM kata ya
Mlangarini wanaotajwa kuwa karibu na marehemu wakati wa uhai wake
walionyeshwa kushtushwa na tukio hilo ambapo walikutwa wakitafakari nje
ya hoteli hiyo.
Uongozi wa hoteli
hiyo ulipotafutwa ili kutoa ufafanuzi juu ya tukio hilo uligoma
kuzungumzia kwa madai kwamba limefikishwa mbele ya vyombo vya usalama.
Bertha blog inatoa pole kwa CCM pamoja na familia ya mareham Benson,
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE
amina
0 comments:
Post a Comment