Nairobi, Kenya
JOPO la Majaji sita nchini Kenya leo wanatarajia
kuweka historia
mpya watakapokuwa wakiandaa uamuzi wa uhalali wa uchaguzi Mkuu
uliofanyika Machi 4 mwaka huu.
Watu mbalimbali ndani nan je ya nchi hiyo watafuatilia kesi hiyo
iliyofunguliwa na Mgombea wa Muungano wa CORD Raila Amolo Odinga ya
kupinga matokeo ya Urais yaliyomuweka Uhuru Kenyatta madarakani.
Uamuzi wa Jopo la Majaji sita wa Mahakama ya Juu nchini humo ndiyo
itakayo maliza ubishi kama Kenyatta ataendelea kubaki Ikulu ama atarudi
kwenye Uchaguzi huo.
Huu ni uchaguzi wa kwanza nchini Kenya kupingwa Mahakamani chini ya Katiba Mpya ya nchi hiyo.
Odinga alifungua kesi katika Mahakama hiyo baada ya kudai kwamba
haridhiki na matokeo ya Urais kutokana na wizi wa kura uliofanywa na
Mgombea wa Jubilee Uhuru Kenyatta.
0 comments:
Post a Comment