.

.
Monday, March 4, 2013

10:39 PM

  Rais mstafu  wa Kenya Mwai Kibaki na kitandawili  cha nani kumkabidhi Ikulu

 Kampeni  za uhuru  Kenyata  zilizofanyika  Kenya

Uhuru Kenyeta akipungia mkono  wafuasi  wake

Baadhi ya ujumbe mbalimbali kwenye moja ya mitaa wenye kuhamasisha amani wakati wa uchaguzi mkuu Kenya.
Wakati matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Kenya yakionyesha kuzidi kumpata ushindi uhuru Kenyata kwa asilimia 57.51 dhidi ya Raila Odinga anayefuatia kwa asilimia 38.55.
Watu wenye silaha ikiwemo mishale, wamewavamia na  kuwaua watu sita wakiwemo polisi wanne, waliokuwa kwenye doria kwenye eneo la Changamwe, Mombasa nchini Kenya.

Hadi jana Saa 6:00 usiku, Uhuru Kenyatta alikuwa akiongoza kwa kupata zaidi ya asilimia 56 za kura zilizokuwa zikihesabi huku akifuatiwa na Raila Odinga aliyepata zaidi ya asilimia 39. Matokeo yalikuwa yakiendelea kutangazwa kadri yalivyokuwa yakipatikana.

Mkuu wa Polisi wa nchini hiyo, David Kimaiyo, alisema jana kuwa, polisi hao na watu wengine walipoteza maisha Jumapili usiku, wakati askari walipopambana na kundi la watu waliokuwa wakienda kuvamia Kituo cha Polisi Mombasa.

Kimaiyo alisema, wavamizi hao wanasadikiwa ni  wanachama wa kikundi haramu cha MRC, na katika mapambano hayo silaha mbili za Polisi zilipotea.

Alisema, saa tatu usiku Jumapili, Polisi walipata taarifa kuwa kuna watu walipanga kwenda kuvamia Kituo cha Polisi cha  Kona, na ilipofika saa tano usiku, kundi la watu zaidi ya 200 walikuwa njiani kwenda kwenye kituo hicho.

Kutokana na hali hiyo, alisema Polisi iliamua kupambana nao ikiwa ni pamoja na kupeleka askari 400 jana.

Alisema, polisi wameruhusiwa kutumia nguvu kutuliza vurugu na wametakiwa kuhakikisha hakuna askari au mwananchi anauawa.  Ameomba ushirikiano wa wananchi ili kuimarisha ulinzi.

“Maofisa wa Polisi wamepoteza maisha yao wakati wanalinda nchi,” alisema Kimaiyo na kuhamasisha wananchi waende kupiga kura kwa kuwa ulinzi umeimarishwa. 

Kimaiyo alisema, wavamizi hao wakiwa na silaha ikiwemo mishale, waliwazidi nguvu polisi, wakaumizwa sana, na baadaye askari hao walipoteza maisha. 

Kwa mujibu wa Polisi, baadhi ya wavamizi waliokufa katika mapambano hayo, wawili walikamatwa na sasa wanasaidia uchunguzi. 

Taarifa ambazo hazijathibitishwa na Polisi, zimeeleza kwamba wavamizi sita wa MRC walikufa katika mapambano hayo.

Kimaiyo alisema, Polisi wameimarisha ulinzi katika Jimbo la Pwani ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwa askari 400 jana.

Mgombea urais wa Kenya katika uchaguzi, Peter Kenneth, alisema jana kuwa tukio hilo la Mombasa ni la kigaidi na akatoa pole kwa familia za polisi waliopoteza maisha.

Mgombea mwingine wa urais, Uhuru Kenyatta, alisema jana kuwa, yaliyotokea Mombasa yanasikitisha, na akawasihi wananchi waende kupiga kura, wakimaliza waende nyumbani kusubiri uamuzi wa Wakenya.


Matokeo haya hadi saa 8.49 usiku Uhuru Kenyata  alikuwa amepata  kura 502,222 sawa na asilimia 57.51 na mpinzani  wake mkuu Raila Odinga alikuwa na kura 340,027 sawa na asilimia 38.55

0 comments:

Post a Comment