MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo na (Chadema) Wilfred Lwakatale ameachiliwa uhuru na Mkurugenzi wa Mashataka nchini (DPP),Dk.Eliezer Feleshi na kukamatwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
DPP alitupilia mbali mashtaka hayo baada ya upande wa mashtaka kufanya kosa la kuwahoji washtakiwa hao kama wanakubaliana na makosa hayo ama wanapinga.
Kosa hilo lilitosha kumfanya DPP kufuta mashtaka ya ugaidi yanayowakabili watuhumiwa hao kwa sababu Mahakama hiyo haina uwezo wa kuwahoji watuhumiwa wala kusikiliza kesi hiyo.
Washtakiwa hao waliachiwa huru jana nyakati za saa 3 asubuhi na Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Prudence Rweyongeza kuwasilisha hati toka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), akiiomba mahakama kuwaachia chini ya kifungu cha 91 (1).
Rwenyongeza alisema kifungu hicho, cha 91 (1) kinampa mamlaka (DPP),Dk.Feleshi kumuachia mshtakiwa yoyote pale anapoona hana sababu ya kuendeleza mashtaka dhidi yake bila hata ya kutoa sababu zilizilizopelekea kufanya hivyo.
Baada ya kuwasilishwa kwa hati hiyo ya DPP, Hakimu Mchauru alikubaliana nayo na kuwafutia mashtaka washtakiwa hao waliokuwa wanakabiliwa na kesi namba 37 ya mwaka 2013, iliyokuwa na mashtaka manne.
Mashtaka hayo ni pamoja na kula njama ya kutenda kosa la kutaka kumdhuru Dennis Msacky kwa sumu, kushiriki kupanga njama za utekaji nyara, kushiriki katika mkutano wa kupanga kitendo cha ugaidi cha utekaji nyara na kuhamasisha vitendo vya ugaidi.
Kabla ya kufutwa kwa kesi hiyo, Hakimu Mchauru alitakiwa kutoa uamuzi wa kama washtakiwa hao watapata dhamana ama la kutokana na hoja zilizokuwa zimewasilishwa na mawakili wa pande zote mbili.
Washtakiwa hao wa kesi ya ugaidi walisomewa mashtaka hayo na kurudishwa lumande mpaka April 3 mwaka huu kesi hiyo itakapo somwa tena mahakamani hapo,hata hivyo washtakiwa hao walinyimwa dhama na kutokuruhusiwa kusungumza chochote kwakuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za ugaidi.
0 comments:
Post a Comment