Mechi
ya kwanza ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za
Afrika 2015 nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe
(Mighty Warriors) itafanyika Jumapili (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
Awali
mechi hiyo tulipanga ichezwe Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa nia ya
kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa
mechi za kimataifa.
Ili
Uwanja wa Sokoine uweze kuchezwa mechi za kimataifa za mashindano,
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilituma Mkaguzi (inspector)
wake kwenye uwanja huo Jumamosi (Mei 10 mwaka huu) ambapo imeamua kuwa
marekebisho yanayofanyika hayatamalizika katika muda stahili, hivyo
mchezo huo kutochezwa Sokoine.
Tunatoa
mwito kwa wamiliki wote wa viwanja kuwasiliana na TFF ili Idara ya
Ufundi iwaelekeze maboresho ya kufanya ili viwanja vingi iwezekanavyo
viweze kukidhi viwango vinavyotakiwa na CAF na Shirikisho la Kimataifa
la Mpira wa Miguu (FIFA).
Taifa Stars ambayo ilikuwa kambini mkoani Mbeya itarejea Dar es Salaam keshokutwa (Mei 14 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment