SIKU zinazidi kusogea huku tambo za kisiasa zikizidi kuhusu
nafasi ya vyama vya siasa katika uchaguzi mkuu wa 2015. Tambo hizo hasa
ni kwa vyama vikubwa – CCM na Chadema.
Chadema
kimeanza kuandaa mashambulizi ya kuchukua madaraka ya nchi kutoka
mikononi mwa CCM, lakini hiyo haitakuwa kazi rahisi kwa kuwa CCM nayo
inaelekeza mashambulizi kwa Chadema kama chama, na wanachama binafsi,
hasa Dk Willibrod Slaa ambaye jina lake limeendelea kusimama kama alama
ya chama hicho.
Chama
hicho kimetokea kuwa ni mwiba mkali kwa CCM, na kuwa kivutio kwa idadi
kubwa ya vijana kutokana na ushawishi unaojidhihirisha kutoka kwa
wabunge na makamanda wa chama hicho.
Mbali
na ushawishi huo, pia chama hicho kimekuwa kikijivunia mipango yake
mahususi, kama operesheni za ujenzi wa chama, kurudisha madaraka kwa
wanachama kupitia Sera yake ya majimbo na shughuli zingine.
Januari
27 na 28, mwaka huu chama hicho kimefanya vikao vyake vya juu – Kamati
Kuu na Baraza Kuu – na kujadili ajenda mbalimbali ikiwa ni sehemu ya
mkakati wa kuhakikisha kinashinda Uchaguzi Mkuu 2015.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika
hatua iliyopo ni kuzingatia uamuzi ya kuwapata viongozi na kuweka
mpango kazi wa kuongeza nguvu ya umma.
“Tunaanza
ujenzi wa chama ili kujiimarisha zaidi katika harakati za kushinda
uchaguzi mkuu ujao, lakini pia tunajiweka sawa kwa namna
tutakavyosimamia ahadi zetu za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwa
kuishinikiza Serikali kutekeleza,” anasema Mnyika. Kwa upande wake
Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ametangaza vita ya kisiasa,
akisisitiza kuwa “Mwaka 2013 ni mwaka wa nguvu ya umma.”
Anasema
chama hicho kimeweka mikakati ya kujijenga kuanzia matawi hadi taifa na
kutawashughulikia wanachama wanaodaiwa kutumiwa na CCM kuanzisha
migogoro ndani ya chama.
Kauli
hiyo ya mwenyekiti, ni kinaashiria kuwa ndani ya chama hicho kuna
migogoro ambayo isipoangaliwa na kutatuliwa katika kipindi hiki,
wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema inaweza kuwa kikwazo kwa
harakati na mipango yake ya kushika dola.
Uamuzi kufuata Katiba
Profesa
Chris Maina wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anasema Chadema inapaswa
kuhakikisha inafanya uamuzi na kutekeleza mipango yake kwa kufuata
Katiba, ili kuhakikisha inaendelea kuimarika zaidi mpaka kufikia
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Anasema
endapo migogoro inayodaiwa kuwamo itaendelea ndani ya chama hicho, na
chenyewe kikafanya uamuzi bila kufuata katiba yake, basi hakutakuwa na
mafanikio ndani ya chama hicho.
0 comments:
Post a Comment