mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Salum Kidima (wa tatu kulia na kushoto) akiwa katika pozi na wanachama wa CCM |
Vijana wa Chama cha Mapinduzi( UVCCM) wametakiwa kusimamia
nafasi zao vema ili kufanikisha CCM kuchukua viti vyote kwenye uchaguzi wa
vitongoji na vijijimwaka 2014 sambamba na viti vya majimbo na hata Urais katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Hayo yametolewa na katibu Umoja wa vijana wa CCM bwana Salum
Kidima alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa uchaguzi wa umoja huo kama mgeni rasmi ulofanyika huko wilayani Monduli Mkoani
Arusha.
Kidima alisema kuwa kwa kuwa vijana ndio chanzo cha
maendeleo yeyote katika mataifa mbalimbali duniani hivyo na vijana wa chama cha
Mapinduzi amewataka wawe chanzo cha maendeleo ya CCM kwa kusimamia nafasi zao
vema kuhakikisha chaguzi zote kuanzia ngazi ya vijiji, vitongoji, kata, majimbo
na hata kiti cha Urais wanaongoza kwa kushinda nafasi hizo.
Aidha mkutano huo wa uchaguzi uliokuwa na wajumbe 275 wa
chama cha mapinduzi ulifanikiwa kumchagua Amani Loiboni kama mwenyekiti wa
UVCCM wilaya ya Monduli kwa kura 172 ambapo alimbwaga mpinzania wake wa karibu
kabisa Seuri Mollel aliyepata kura 102.
Pia Umoja huo ulibahatika kuwapata wajumbe wa viti vya
utekelezaji wa Wilaya ambao ni Gasper Mollel, Lina John, Namnyaki Mollel pamoja
na Lesikar Mepokori.
0 comments:
Post a Comment