TIMU ya
Yanga leo imepunguza kasi yake kwenye ligi kuu ya Vodacom baada ya
kulazimisa sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro katika mchezo
ulipigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika
mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa,Mtibwa ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata
bao lake katika dakika ya 44 kupitia kwa Shaban Kisiga aliyeunganisha kwa
kichwa kona ya Issa Rashid alikipokea pasi ya Osacr Joshua.
Kipindi cha
kwanza cha mchezo huo, timu zote ziulifanya mashabulizi ya kupokezana . huku
Yanga ikipoteza nafasi za wazi kupitika kwa wachezaji wake Didier Kavumbagu,
Jerry Tegete na Simon Msuva, huku Mtibwa nao wakipoteza kupitia kwa Kisiga,
Rashid Gumbo, Vicent Barnabas na Hussin Javu.
Hata hivyo,
timu hizo zilikwenda mapumziko kwa Mtibwa kuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kila timu kucheza kwa kasi zaidi huku Yanga ikionekana na
uchu wa kutaka kufunga mabao lakini safu ya ushambuliaji ilishindwa kutikisa
nyavu za Mtibwa Sugar.
Hamis Kiiza
aliisawazishia Yanga bao katika dakika ya 84, huku Yanga ikiutawala zaidi
mchezo huo.
Kwa matokeo
hayo Yanga inaendelea kuongoza ligi hiyo kwa pointi 33 huku Azam Fc inayoshika
nafasi ya pili kwa pointi 30.
Yanga:Ali
Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin
Yondan, Athuman Iddy ‘Chuji’, Frank Domayo, Simon Msuva, Didie Kavumbagu, Jerry
Tegete na Haruna Niyonzima.
Mtibwa:Hussin
Sharif, Said Mkopi, Issa Rashid, Rajab Mohammed, Salum sued, Shabn Nditi,
Vicent Barnabas,Rashid Gumbo, Hussein Javu, Shaban Kisiga na Ally M ohammed.
0 comments:
Post a Comment