WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wa Kijiji cha Shambarai Simanjiro Mkoa wa Manyara wametishia kuhama
chama hicho baada ya baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kudaiwa kuuza
maeneo ya wazi bila utaratibu.
Wakizungumza
na waandishi wa habari juzi,wanachama hao waliogoma kutaja majina yao,
walisema wamefikisha kilio chao kwa uongozi wa CCM wa kata hiyo kwa
kuwa viongozi wa kijiji wameto CCM lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.
Walisema
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho,Edward Wazi na Ofisa Mtendaji wa
kijiji hicho, Mosses Peter wamewauzia sehemu ya malisho matajiri kutoka
Arusha bila kufuata utaratibu wa kuidhinishwa na mkutano wa kijiji.
Walisema
viongozi hao wameuza maeneo ya kijiji chao ikiwamo mapalio ya
kupitishia mifugo na wakihoji kwa viongozi hao kwa nini wameuza maeneo
yao wanatishiwa kwa maneno hivyo wanashindwa mahali pa kwenda
kulalamika.
“Tumefikisha
suala hilo kwa kulalamikia hadi kwenye ofisi ya CCM ya kata,kwani
viongozi hawa wa kijiji wamechaguliwa kupitia chama kilichpo
madarakani,lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yao,”
walisema wakazi hao.
Walisema
maeneo hayo yaliyouzwa yaliachwa tangu mwaka 1975 kwa ajili ya maeneo
ya kupitishia na kulishia mifugo,lakini wameshangazwa na viongozi hao
kuamua kuyauza kwa wafanyabiashara hao kutoka Arusha.
Hata
hivyo,Mwenyekiti wa kijiji cha Shambarai,Edward Wazi na Ofisa Mtendaji
wa kijiji hicho,Mosses Peter walikanusha vikali kuuza maeneo hayo ila
walidai kuwa yameuzwa na wamiliki husika wa maeneo hayo hivyo wao
hawahusiki.
Wazi
alisema maeneo hayo siyo ya Serikali ila wamiliki wenyewe wameyauza
mashamba hayo ambayo ni mali yao na wao hawana mamlaka ya kuingilia au
kutoa uamuzi juu ya mashamba hayo.
Peter
alisema wamiliki hao wameyauza kihalali mashamba hayo baada ya kupata
shida, hivyo wao hawana uamuzi wa kumzuia mtu kuuza eneo lake kwani
wenyewe hawamiliki chochote na wala hawahusiki na
ashamba hayo
-->
ashamba hayo
0 comments:
Post a Comment