.

.
Friday, February 1, 2013

12:02 PM

                                                     Na Mohamed Isimbula-Dongobesh
wakina mama wa kata ya dongobeshi wilayani mbulu wamemuomba kamanda wa polisi mkoa wa manyara Akili Mpwapwa kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya asikari wa kituo cha mbulu akiwemo mkuu wa kituo hicho kwa madai ya kuwapinga na kusababisha baadhi yao mimba zao kuharibika

Wakizungumza mbele ya mkuu wilaya hiyo Anatori Choya akina mama hao wapatao sita akiwemo bibi kizee  miaka 85 anayefahamika kwa jina la Fabrinia Gusolo alisema polisi hao wakiongozwa na mkuu huyo waliwafata wamama hao katika majumba yao mwazoni mwa wiki kwa madai kuwa kwa nini wamama hao walishiriki katika kikao cha mila za wairagw kinyume na taratibu 
 Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mtendaji wa kata hiyo wamama hao pia walimueleza mkuu huyo wa wilaya kuwa katika taharuki hiyo iliyofanwa na poilsi hao kuanzia saa sita za usiku pia zilipekea wanawake wengine ambao umri wao ni mdogo kutokwa na damu katika sehemu za siri kwa muda wa siku tatu huku wakiwa chini ya ulinzi wa polisi kituo cha mbulu

Huku akitokwa na machozi  mbele ya mkuu wa wilaya hiyo mmoja wa wahanga wa tukio hilo Scola jemsi ambaye pia anauguwa ugonjwa wa kifafa alisema kutokana na kipigo alichokipata toka kwa polisi hao ikiwa ni pamoja na kumdhalilisha kwa kumvua nguo na kubakia na nguo za ndani kulisababisha pia mtoto wake wa mwaka moja kuacha kunyonya kutokana na yeye kukaa polisi siku tattu bila mtoto huyo kunyonya
Naye Yasinta Amosi  akizungumzia hali hiyo alisema polisi hao ambao hawakuwa na polisi wa kike katika tukio hilo, walidhalilishwa kwa kushikwa tanganyika jeki hali ilyosababisha baadhi yao kubakia uchi.


“tunajua kama sisi tulikuwa na makosa ilipaswa polisi wa kike waje kutukamata lakini sheria hiyo hakufuatwa na sasa baadhi yetu  mimba zao zimetoka na wengine kuharibika kutokana na kukanyagwa na polisi usiku huo alilalamika  Yasinta 
Anatori Choya ni mkuu wa wilaya ya mbulu akijibu hoja za akina mama hao alisema kutokana na makosa hayo yaliyofanywa na jeshi hilo uchunguzi utafanyika na iwapo kutabainika baadhi ya askari hao kuwadhalilisha wanawake hao hatua kali zitachukuliwa dhidi yao 
Kuhusu mimba zilizoharibika kutokana kipigo hicho mkuu huyo aliwataka wale wote ambao mimba zao zimeharibika wafike kituo cha polisi mbulu na waweze kufunguwa mashitaka dhidi ya askari hao iwapo wanawafahamu

“Naagiza kuwa kama munawafahamu askari hao kafuguweni kesi na kama polisi watawakatalia kufanya hivyo njooni ofisini kwangu tutakwenda na mimi siwezi kuona kazi zinafanywa kinyume halafu ninyamaze alifoka mkuu huyo
Pia mkuu huyo alimtaka  mkuu wa polisi wilaya hiyo kumpatia maelezo ni kwa nini hakuwa na askari wa kike katika kazi hiyo ya kuwakamata wamama hao na hivyo kufanya kazi bila kuzingatia maadili na sheria za kazi
Kamanda wa polisi mkoa wa manyara Akili Mpwapwa ameahidi kufuatilia tatizo hilo na kuchukuwa hatua za kisheria

0 comments:

Post a Comment