.

.
Tuesday, February 19, 2013

5:27 AM
TANZANIA CHRISTIAN FORUM (TCF) MKOA WA MBEYA
TAMKO RASMI KUTOKA KTK JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA
MHESHIMIWA NDG. ABAS KANDORO,
KAMA MKUU WA MKOA NA MWAKILISHI WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE MKOA WA MBEYA, TUNAPENDA KUSOMA MBELE YAKO TAMKO RASMI LA JUKWAA LA WAKRISTO MKOA WA MBEYA (TCF).
NDUGU MKUU WA MKOA,
            “HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU WOWOTE” (Mit. 14:34).
Katika mkutano wa jukwaa la Wakristo Tanzania mkoa wa mbeya ulionyika tarehe 12/02/2013 Jijini Mbeya, wajumbe tulitafakari kwa undani juu ya hali inayoendelea kujitokeza katika nchi yetu na hasa katika mahusiano baina ya dini mbili kuu UKRISTO NA UISLAMU.
Jukwaa hilo lilijumuisha taasisi zake kuu (yaani mabaraza ya Madhehebu ya Kikristo)
Tanzania Episcopal Council (TEC), Christian Council of Tanzania (CCT) na Pentecostal Council of Tanzania (PCT).Mbali na mambo yake ya kawaida jukwaa hilo lilitafakari utekelezaji wa Serikali juu ya tamko Rasmi la jukwaa la Wakristo kitaifa lililotolewa tarehe 06/12/2012 na kusomwa katika makanisa yote ya Kikristo nchini kwenye sikukuu ya Krismas tarehe 25/12/2012. Katika tafakari letu jukwaa la Wakristo wa Mkoa wa Mbeya tumeona kuwa kunabaadhi ya mienendo inayojitokeza katika nchi yetu ambayo kama isipodhibitiwa na kukomeshwa na Serikali italeta athali kubwa na hata kuondoa amani na uthabiti (Stability) wan chi.
Katika kutafakari kwa jukwaa juu ya athari zinazoweza kujitokeza, kumekuwepo na mambo yanayotendeka waziwazi yenye athari kubwa kwa amani na usitawi wa nchi na wananchi wake kwa ujumla. Kwa mfano, uchochezi, kashfa, matusi na uchokozi wa wazi unaofanywa na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupitia vyombo vya habari vya kidini (rediona magazeti), mihadhara, kanda za video, CD na DVD pamoja na kauli zinazotolewa na viongozi wa dini hiyo kwenye baadhi ya nyumba zao za ibada(ushahidi upo kama vile uhamasishaji wa Sheikh Ilunga) pasipo serikali kuchukua hatua stahiki na badala yake kubaki kimya au kupambana na wanaofichua harakati hatarishi kwa utulivuwa nchi.
Miongoni mwa harakati hatarishi zinazosambazwa kwa njia ya CD na DVD za Sheikh Ilunga, kuhusu kuua Wachungaji, Mapadri na Maaskofu zimeanza kuwa matokeo mabaya; kwani Padri kule Zanzibar alipigwa risasi na watu walioitwa na serikali wahuni na sasa kifo
Kimetokea na mchungaji Mathayo Kachila kule Buselesele Mkoani Geita na kikundi kinacho dhaminiwa ni wanaharakati hao wa kiislamu wenye jazba na gadhabu kali inayotokana na mvutano uliopo kati ya wakristo na waislamu kuhusu nani mwenye haki kisheria KUCHINJA WANYAMA. Hatua zinazochukuliwa na Serikali hazilizishi wala kukidhi matakwa ya wananchi wapenda amani. Tuna mifano kadhaa ya matukio kama haya yaliyojitokeza kwa wanchi wenzetu moja ni ile ya mwenzetu aliyepigwa risasi kule Rungwe Ndg. John Mwankenja (Mwenyekiti wa CCM Rungwe) aliyepigwa risasi kwa mambo yanayodhaniwa kuwa ni ya kisiasa) Serikali ichukuwe hatua madhubuti kwa kutuma wachunguzi kutoka Dar es salaam kwa swala hilo na wote tuliridhika kwa hatua hizo madhubuti. Hatua kama hizo mbona hazichukuliwi katika masuala haya ya kidini na badala yake Serikali inakaa kimya au inachukua hatua ambazo kimsingi hazitatui tatizo ili wananchi waridhike na Serikali yao? Je tuseme Serikali inaangalia haiba (Personality) za watu au aina ya vikundi? Swala la uchinjaji lilipo jitokeza kule Mwanza waziri wa nchi ndg. Steven Wasira alienda na kutoa majibu mepesi katika swala zito je, tuseme aliyoyatamka huko yalikuwa ni KAULI YA SERIKALI au kauli yake mwenyewe? Na kama yake mwenyewe mbona Serikali haijakanusha waziwazi? Na kama ni kauli ya serikali hiyo haki ya kuchinja kwa waislamu inatokana na sheria zipi za nchi? Je huo ndio utawala wa sheria tuliyoahidiwa na serikali ya awamu ya nne kuwa itatenda kazi kwa kuzingatia utawala wa sheria.
Kupigwa risasi kwa Padri na kuuwawa kwa mchungaji kunathibitisha azma halamu na batili ya “Ua, chinja” mapadri, wachungaji na maaskofu iwe kwa siri au kwa wazi iliyoasisiwa na Sheikh Ilunga ambayo sio tu inahatarisha amani ya nchi lakini pia inavunja haki za kuishi za binadamu zilizoainishwa katika katiba ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha harakati hizi zina muelekeo wa kudhoofisha ukristo Tanzania kama sio kuumaliza kabisa. Pamoja na mambo mengine kinachosikitisha ni namna ambavyo serikali inavyoyashughulikia mambo mazito yanayotikisa amani na utulivu wa nchi. Utasikia mala ikisema “Mtu haruhusiwi kujichukulia sheria mkononi” na ndipo kikundi fulani kitaibuka na kuvunja mabucha na kuchoma nyama iliyomo humo hapo tena utasikia serikali hiyohiyo ikitoa kauli kwamba “Mvumiliane” je tunakwenda wapi?
Kwa misingi hiyo kwa nini tusite kusema kwamba serikali ya chama cha mapinduzi (CCM) inaibeba dini ya kiislamu? Kwa kuwa jukumu la serikali ya chama cha mapinduzi ni kuhakikisha kuwa wananchi wote wa Tanzania bila kujali dini zao, makabila yao na hata rangi zao wanaishi katika misingi ya uhuru, haki, udugu na amani kama raisin a watendaji wake walivyotoa kiapo mara baada ya kupewa dhamana ya kuiongoza nchi na wananchi wake kwa ujumla pasipo na ubaguzi wowote.
HITIMISHO: Ili wakristo wote nchini warudishe imani yao kwa serikali ya chama cha mapinduzi mambo yafuatayo ni lazima yachukuliwe hatua za haraka iwezekanavyo:    
  1. Tunataka Serikali izingatie utawala washeria kulingana na ahadi yake katika kushughulikia maswala ya kijamii na sio vinginevyo. Kwa kuzingatia sheria maswala ya imani na dini yapo wazi kabisa kama zilivyoanishwa kwenye katiba ibara ya 19 (1), (2) (3) (4)  na kufanya vinginevyo ni uvunjifu wa sheria.
  1. Swala la kuua lisichukuliwe kama mazoea ya kawaida na inapotokea popote ni lazima Serikali ichukuwe hatua inayostahiki kwa kuzingatia utawala wa sheria kwa kuwa wote wako sawa mbele ya sheria ibara ya 12, 13 (1) –(5).Usawa huo ni lazima uonekane katika swala la mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila na kama hatua zilivyochukuliwa katika mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa halmashauri na mwenyekiti ya CCM Wilaya ya Rungwe Ndg. John A. Mwankenja. Hiyo ni haki ya msingi kkwa kila mtantania bila kuangali haiba (Personality) yake kama katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania inavyoainisha haki xza kuishi, kulindwa na kushughuklikiwa kisheria katika ibara ya 14 na 15 pamoja na vifungu vyake viwili vidogo.
  2. Tunataka Serikali itueleze ni ushahidi gani zaidi inaoutaka kuliko ule unaopatikana kwenye CD na DVD zilizotolewa na Sheikh Ilunga kama inazingatia utawala wa sheria.
  3. Tunataka Serikali iwajibike kutolea ufafanuzi kauli ya waziri wa nchi Ndg. Steven Wasira inayohusu haki ya kuchicha kwa waislamu kama inatokana na sheria gani ya nchi?
  4. Kama Serikali inatekeleza utawala wa sheria, tunataka wakristo tuwe na machinjio na bucha zetu kulingana na imani yetu.
  5. Kama Serikali haitachukuwa hatua za makusudi katika kutekeleza madai yetu sisi kama viongozi wa dini ya kikristo tutachukua hatua ya kuwaambia waumini wetu kwamba Serikali ya chama cha mapinduzi inaibeba dini ya kiislamu na wao watajua la kufanya.
Pamoja na kutaka utekelezaji wa haraka kutoka kwa Serikali bado tunawaomba wakristo tuwe katika hali ya maombi na utulivu kwa wakati huu ambapo tumo katika vita vya kiroho ili Mungu akatuimarishie amani ambayo ni nguzo kuu ya Taifa letu. Tamko hili rasmi la jukwaa la wakristo Mbeya lisomwe katika makanisa yetu yote siku ya juma pili tarehe 24/02/2013.
Tunakuambatanishia na nakala ya Tamko Rasmi la TCF Taifa la tarehe 6/12/2012.
NDUGU MKUU WA MKOA NAWASILISHA.
Nakala kwa:
  1. Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
  2. Tanzania Christian Furum Taifa
  3. Mwenyekiti wa the Tanganyika Law Society.
  4. Vyombo vya habari TV, Redio na magazeti

0 comments:

Post a Comment