.

.
Thursday, February 21, 2013

11:20 AM

Shirika la nyumba la Taifa limeweka mikakati ya kupunguza mahitaji ya nyumba zaidi ya milioni 3 hapa nchini kwa kuhakikisha wanajenga nyumba zaidi ya elfu 3 kila mwaka.
Hali itakayowasaidia watanzania wengi kumiliki nyumba zao.
`          
Hayo yamelezwa na Waziri wa Ardhi,nyumba, na maendeleo ya
makazi,Profesa Anna Tibaijuka hivi karibuni  wakati akizundua mradi wa nyumba za
makazi katika eneo la Levolosi ambazo zimejengwa chini ya Shirika la
nyumba sambamba na hoteli ya palace iliyojengwa kwa ubia wa NHC pamoja kampuni ya palace.
Tibaijuka alisema kuwa  mahitaji hayo ya nyumba kila mwaka
yanaongezeka kwa kiasi cha nyumba laki tatu lakini ongezeko hilo ni
lazima liweze kupunguzwa tena kwa haraka sana kwa kubuni aina
mbalimbali ya nyumba ambazo zitarahisisha makazi bora na imara

Aliongeza kuwa Hitaji ni kubwa sana la nyumba hapa nchini hivyo
jitiada za haraka sana zinahitajika katika kuhakikisha kuwa hata
nyumba ambazo zinajengwa ziweze kuwa imara na ziweze kuwasaidia hata
zaidi wananchi wa vijiijini ambao mara nyingine wanaonekana kukosa
nyumba bora na imara

Alisema kuwa kama Shirika hilo amblo kinaendeshwa lenyewe litaweza
kuwa bunifu na kujenga nyumba nyingi zaidi basi litachangia kwa
kiwango kikubwa sana ongezeko hilo la nyumba zaidi ya Laki tatu kwa
kila mwaka kuweza kupungua na hata baadhi ya miji kuweza kupangika kwa
uraisi sana

“Tanzania kwa sasa tunakabiliwa na changamoto hii lakini ni vema sasa
Shirika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tukahakikisha kuwa
tunasonga mbele zaidi na hata kuangalia jinsi ya kupunguza tatizo hilo
ambalo kama halitaaweza kutatuliwa kwa uraisi basi litasababisha
madhara kwa kuwa wapo baadhi ya watu ambao watakosa sehemu za
kuishi’aliongeza Tibaijuka

Katika hatua nyingine alisema kuwa nao wanasiasa wana nafasi kubwa
sana ya kushirikiana na Shirika hilo kwa kuwa bado shirika hilo
linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile kushindwa kujenga
kutokana na Ardhi ambayo inauwza kwa bei ya juu sana lakini kama
watasaidiana basi wataweza kutatua changamoto hiyo ambayo nayo
inafanya shirika hilo kushindwa kuendelea kujenga nyumba nyingi zaidi

Awali mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Nehemia Mchechu alisema kuwa ili
kukabiliana na tatizo hilo la ongezeko la mahitaji ya Nyumba  hapa
Nchini Shirika hilo limeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa
mpaka 2014 watakuwa tayari wameshajenga nyumba 15,000.

Mbali na hayo alisema kuwa kwa Mkoa wa Arusha wanatarajia kuanza
kujenga nyumba za garama nafuu katika wilaya ya Arumeru pamoja na
Arusha huku lengo halisi likiwa ni kuhakikisha kuwa mji wa Arusha
unaendelea kuboreka zaidi kwenye hadhi za kimataifa na kuachana na
ujenzi holela ambao mara nyingine unasababisha ukosefu wa nyumba.

Alisema nyumba hizo zitajengwa  maeneo ya Arusha,Dar es Salaam, Mbeya ,Mwanza na
sehemu mbalimbali za Tanzania ambapo  NHC imepata ekari 3000 Wilayani Arumeru Mashariki, eka 600 eneo la Burka na Arusha Mjini hivyo wanaeka 28,000 na kwa nchi nzima ambayo ni kwaajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya ujenzi.

Naye Mkurugenzi wa Hoteli ya Palace Jijini Arusha,  Hans Macha alisema
kuwa hoteli hiyo yenye ubia na shirika la nyumba na kampuni ya palace ilianza kujengwa rasmi mwaka 2008 na kumalizika 2011 ambapo liligharimu jumla ya shilingi bilioni 16 za kitanzania na wanatarajia kuajiri wafanyakazi rasmi 120 na wengine wasio rasmi.

Kwa upande wake mwenyeji wa waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema aliishukuru shirika hilo na uongozi wa Palace kwa kujenga hoteli hiyo na kuahidi kutunza Amani ya Jiji ili kupata wageni wengi zaidi na kuwataka viongozi wa Mkoa kutenda haki itakayotekeleza upatikanaji wa Amani hiyo.

“Kwa kiongozi yoyote maendeleo kama haya ni ya kufurahia na kujivunia hivyo niwapongeze wote waliofanikisha mradi huu na naahidi kudumisha amani ili kupata wageni wengi zaidi wa kuja kutalii….., lakini siku zote Amani hupatikana kwenye haki hivyo haki ikitendeka Amani huja bila kipingamizi hivyo niombe tu haki itendeke kwa wananchi wetu ili Amani hii iendelee kuwepo.” Alisema Lema




MWISHO

0 comments:

Post a Comment