.

.
Thursday, February 21, 2013

11:18 AM

WAZIRI  wa habari,michezo na Utamaduni,Dkt Fenela Mkangara amezitaka
Halmashauri zote ndani ya mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa zinajiwekea
utaratibu wa kuwa na maafisa Vijana hali itakayowasaidia kuwaunganisha vijana katika  kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali zinawakabili vijana
“zipo Halamshauri ambazo zinakabiliwa na masuala ya changamoto za
Vijana lakini hakuna afisa yoyote ambaye  ana uwezo wa kutatua kero za
vijana hivyo asilimia kubwa ya vijana wanabaki wakiwa  wanalalamika
ovyo juu ya Serikali”

Mkangara aliyasema hayo wiki hii Jijini hapa wakati akiongea na
viongozi mbalimbali wa Jiji la Arusha akiwemo Mkuu wa Wilaya kuhusiana
na maendeleo ya Vijana pamoja na changamoto,utatuzi wake kwa kipindi
miaka iliyopita.

Dkt Fenala alisema kuwa endapo kama Halmashauri zote za Jiji la
Arusha zitaweza kuwatumia vema hao maafisa Vijana basi zitachangia
sana maendeleo ya Vijana kwa kuwa asilimia kubwa ya vijana wa sasa
wanabaki wakiwa wanalamikia Serikali  kwa kushindwa kuyajua na
kuyatambua mambo ambayo si la kweli

Alisema kuwa kupitia Maafisa Vijana hao ambao wataweza kutatua
changamoto ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati mbalimbali ya vijana ikiwemo ajira
lakini kwa kuwa  kwa sasa hakuna maafisa hao basi Halmashauri zinajitamba
kuwa zinawasaidia vijana hao huku vijana huko mitaani bado wanakabiliwa
na changamoto nyingi sana.

“Wizara yangu imeweka mikakati ya kuondoa matatizo ya vijana lakini
halmashauri pekee haziwezi hii kazi ni nzito jamani ni lazima
mtekeleze ahadi Raisi ya kuwa na maafisa Vijana ambao wataweza
kutukusanyia hawa vijana na kisha hata kama tunakitu cha kuwapa tuweze
kuwapata kwa ukaribu sana na pia hii itasaidia sana vijana hawa waache
kulalamika ovyo:”aliongeza Dkt Fenela

Awali Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongela alisema kuwa tatizo kubwa
la vijana hasa wa mkoa wa Arusha wanachokitaka kikubwa sana ni Pesa na
wala sio mawazo mazuri ya upataji  wa pesa na mitaji imara hivyo bado
asilimia kubwa sana ya Vijana wanabaki wakiwa wanalalamikia Serikali

Mongela alisema kuwa hali hiyo inasababisha vijana kuona kuwa Serikali
haiwathamini,lakini bado Jiji la Arusha limeweka mikakati mbalimbali
ya kuhakikisha kuwa inawapa fursa vijana wa mkoa wa Arusha sanjari na
kuwaboreshea mazingira mazuri na imara ya kufanyia biashara zao pamoja
na shuguli za kila siku.

MWISHO

0 comments:

Post a Comment