.

.
Monday, February 4, 2013

2:44 PM
mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Salum Kidima (wa tatu kulia na kushoto) akiwa katika pozi na wanachama wa CCM

 Vijana wa Chama cha Mapinduzi( UVCCM) wametakiwa kusimamia nafasi zao vema ili kufanikisha CCM kuchukua viti vyote kwenye uchaguzi wa vitongoji na vijijimwaka 2014 sambamba na viti vya majimbo na hata Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


Hayo yametolewa na katibu Umoja wa vijana wa CCM bwana Salum Kidima alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa uchaguzi wa umoja huo kama mgeni rasmi ulofanyika huko wilayani Monduli Mkoani Arusha.


Kidima alisema kuwa kwa kuwa vijana ndio chanzo cha maendeleo yeyote katika mataifa mbalimbali duniani hivyo na vijana wa chama cha Mapinduzi amewataka wawe chanzo cha maendeleo ya CCM kwa kusimamia nafasi zao vema kuhakikisha chaguzi zote kuanzia ngazi ya vijiji, vitongoji, kata, majimbo na hata kiti cha Urais wanaongoza kwa kushinda nafasi hizo.


Aidha mkutano huo wa uchaguzi uliokuwa na wajumbe 275 wa chama cha mapinduzi ulifanikiwa kumchagua Amani Loiboni kama mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Monduli kwa kura 172 ambapo alimbwaga mpinzania wake wa karibu kabisa Seuri Mollel aliyepata  kura 102.


Pia Umoja huo ulibahatika kuwapata wajumbe wa viti vya utekelezaji wa Wilaya ambao ni Gasper Mollel, Lina John, Namnyaki Mollel pamoja na Lesikar Mepokori.

0 comments:

Post a Comment