.

.
Tuesday, February 19, 2013

10:49 PM
WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kijiji cha Shambarai Simanjiro Mkoa wa Manyara wametishia kuhama chama hicho baada ya baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kudaiwa kuuza maeneo ya wazi bila utaratibu.

Wakizungumza na waandishi wa habari juzi,wanachama hao waliogoma kutaja majina yao, walisema wamefikisha kilio chao kwa uongozi wa CCM wa kata hiyo kwa kuwa viongozi wa kijiji wameto CCM lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Walisema Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho,Edward Wazi na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Mosses Peter wamewauzia sehemu ya malisho matajiri kutoka Arusha bila kufuata utaratibu wa kuidhinishwa na mkutano wa kijiji.

Walisema viongozi hao wameuza maeneo ya kijiji chao ikiwamo mapalio ya kupitishia mifugo na wakihoji kwa viongozi hao kwa nini wameuza maeneo yao wanatishiwa kwa maneno hivyo wanashindwa mahali pa kwenda kulalamika.

“Tumefikisha suala hilo kwa kulalamikia hadi kwenye ofisi ya CCM ya kata,kwani viongozi hawa wa kijiji wamechaguliwa kupitia chama kilichpo madarakani,lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yao,” walisema wakazi hao.

Walisema maeneo hayo yaliyouzwa yaliachwa tangu mwaka 1975 kwa ajili ya maeneo ya kupitishia na kulishia mifugo,lakini wameshangazwa na viongozi hao kuamua kuyauza kwa wafanyabiashara hao kutoka Arusha.

Hata hivyo,Mwenyekiti wa kijiji cha Shambarai,Edward Wazi na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho,Mosses Peter walikanusha vikali kuuza maeneo hayo ila walidai kuwa yameuzwa na wamiliki husika wa maeneo hayo hivyo wao hawahusiki.

Wazi alisema maeneo hayo siyo ya Serikali ila wamiliki wenyewe wameyauza mashamba hayo ambayo ni mali yao na wao hawana mamlaka ya kuingilia au kutoa uamuzi juu ya mashamba hayo.

Peter alisema wamiliki hao wameyauza kihalali mashamba hayo baada ya kupata shida, hivyo wao hawana uamuzi wa kumzuia mtu kuuza eneo lake kwani wenyewe hawamiliki chochote na wala hawahusiki na
ashamba hayo
-->

0 comments:

Post a Comment