.

.
Monday, November 25, 2013

10:59 AM
Gervas Kadaga(25) anaetuhumiwa kumuua mkewe akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

MAMA mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina la Martha Lugenge alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja akiwa katika shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.




Mwanamke mkazi wa kijiji cha Mahango kata ya Madibila wilayani Mbarali mkoani Mbeya aliyefahamika kwa jina la Jitihada Mamga(20) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe aliyefahamika kwa jina Gervas Kadaga(25) ambaye pia ni mkazi wa kijijini hapo.



Tukio hilo limetokea Novemba 21 majira ya saa 1:00 jioni baada ya kutokea ugomvi baina ya wapenzi hao ambapo marehemu alikutwa na majeraha tisa ya kisu katika sehemu mbalimbali za mwili wake.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Bw. Diwani Athumani alisema kuwa marehemu alifia nyumbani kwake ambapo mtuhumiwa ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya naye amejeruhiwa kwa kuchomwa na kisu tumboni.



Hata hivyo Kamanda Athumani alisema kuwa hadi sasa hakijafahamika chanzo halisi cha ugomvi huo ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku mtuhumiwa akiwa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi katika hospitali ya rufaa ya Mbeya alikolazwa.



Akizungumza katika hospitali ya rufaa alikolazwa mama mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha kwa jina la Martha Lugenge alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila mmoja akiwa katika shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.



Alisema yeye alipewa taarifa za tukio hilo siku inayofuata na kwamba alipofika alikuta ndugu wa marehemu wameuchukua mwili wa mtoto wao kwa ajili ya taratibu za mazishi na kwamba hajui chanzo cha ugomvi uliosababisha wapigane visu.



Mama huyo alisema kuwa vijana hao hawajawahi kupata mtoto na kwamba hawajaanza kuishi pamoja muda mrefu; ''Wote ni watoto, kwani wameanza kuishi muda mrefu? wamekutana kila mmoja akiwa katika kazi zake, ndipo walipoanza kuishi kama mke na mume,''alisema  Na Mbeya yetu

0 comments:

Post a Comment