Katibu Mkuu wa ITU ambalo ni Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani Dr. Hamadoun Toure akisikiliza Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni Waziri wa ICT wa Thailand.
Na Innocent Mungy - Bangkok Thailand
Tanzania inashiriki katika Kongano la TEHAMA la Dunia
linaloandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani
(ITU-International Telecommunications Union) linalofanyika katika jiji la
Bangkok nchini Thailand.
Kongano hilo lenye Kauli Mbiu ya Kuchochea Mabadiliko Katika
Ulimwengu wa TEHAMA, unashirikisha nchi wananchama wa ITU na wasio wanachama,
Makampuni ya Mawasiliano Duniani, Taasisi na wasimamizi wa sekta ya Mawasiliano
Pamoja na Serekali, wanashiriki Kongano hili katika kipindi ambacho mabadiliko
makubwa katika Sekta ya Mawasiliano.
Mabadiliko haya yanapelekea dunia kuwa na Changamoto ya
Kuyakubali Mabadiliko hayo na kukabiliana na Changamoto zake kwani faida za
mabadiliko ni kubwa kwa Jamii Habari duniani. Akizungumza jijini Bangkok,
Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa amesema
Tanzania iko tayari kwa na imeshapokea mabadiliko na imetekeleza mikakati ya
kuhakikisha Tanzania inapokuwa mabadiliko bila tatizo.
Aidha Mheshimiwa Mbarawa amesema Tanzania inatambua umuhimu
wa mabadiliko katika TEHAMA hususan kipindi hiki cha dijitali kwani ndio njia
pekee ya kuharakisha maendeleo ya watanzania kwa ufanisi.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma amesema Tanzania
tayari mstari wa mbele kuhakikisha
inachochea mabadiliko ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili wananchi
wafaidike na huduma za Mawasiliano. "Tuna mfumo mzuri wa usimamizi wa leseni
za muingiliano wa teknolojia, sheria na kanuni nzuri ambazo zinawezesha
mabadiliko katika TEHAMA kunufaisha watanzania. Tayari Tanzania imeingia katika
mfumo wa Utangazaji wa digitali na tunaendelea kuweka mazingira mazuri ya
kuwepo kwa huduma nyingi zaidi kurahisisha maisha ya watanzania". Amesema
Profesa Nkoma.
Taasisi kadhaa toka Tanzania zinashiriki Kongano hili kutoka
Tanzania ikiwa ni pamoja na W ziara ya Afya, Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia,
DTBi ya wavumbuzi na wagunduzi, NICTBB inayosimamia mkongo wa Taifa,
MaxCom.
Timu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania katika Maonesho ya ITU Telecom World
Kongano hili linafanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 19 - 22
Novemba 2013. Tanzania inashiriki na kauli Mbiu ya nchi "Tanzania: Africa
Strategic ICT Hub". Pamoja an Kongano pia yako Maonesho ya ICT yenye nia
ya kuonesha jinsi nchi zinavyochochea maendeleo kwa raia wake kupitia TEHAMA.
Banda la Maonesho la Tanzania limevutia watu wengi wanafikia kujifunza jinsi
Tanzania imeweza kuchochea mabadiliko katika TEHAMA na jinsi wananchi
wanafaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa nchini.
Aidha Baadhi ya Taasisi zinazoshiriki zinaangalia uwezekano
wa kuchochea zaidi upatikanaji wa huduma zao kwa kuwa na washirika katika
shughuli zao. Leo asubuhi Ujumbe wa Tanzania ulishiriki katika Mkutano Maalum
wa Wawekezaji Katika Sekta ya Mawasiliano ulioendeshwa na Naibu Katibu Mkuu wa
ITU Bwana Houlin Zhao.
Timu Tanzania I kuifanya mikakati ya kushiriki kikamilifu
katika siku mbili zilizobaki. Hapa wakipeana taarifa ya Matukio ya siku ya
pili.
|
0 comments:
Post a Comment